Wednesday, September 3, 2014
LUKUVI AZOMEWA MBELE YA KIKWETE.
Do you like this story?
Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi amejikuta katika wakati mgumu mbele ya Rais Jakaya Kikwete baada ya kuzomewa hadi kukatisha hotuba yake akipingwa na wananchi pamoja na madiwani wa CCM wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma alipokuwa akitetea kuwapo kwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA).
Lukuvi
alikumbana na mkasa huo wakati akijibu hoja za Mbunge wa Dodoma Mjini (CCM),
David Malole ambaye alitaka CDA ivunjwe akiituhumu kuwavunjia wananchi nyumba
bila kuwatafutia mahali pa kuishi.
Hoja ya Malole
kutaka CDA ivunjwe iliibuka katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata
ya Kikuyu, Manispaa ya Dodoma baada ya Rais Kikwete kuzindua ujenzi wa Barabara
ya Dodoma - Iringa.
Awali, mbunge
huyo akitoa salamu kwa Rais Kikwete, alisema CDA imekuwa ni kero kwa wakazi wa
mji huu.
“Mheshimiwa
Rais, ni bora CDA ikafutwa na ardhi ikarudishwa kwa halmashauri kwa kuwa hakuna
kitu kinachofanyika. Ipo miji mingi ambayo haina CDA lakini imekuwa majiji. Leo
hii zaidi ya miaka 40 CDA imeshindwa kuufanya Mji wa Dodoma kuwa jiji,” alisema
na kuongeza:
“Licha ya kuwa
CDA jukumu lake ni kuhakikisha inapima viwanja na kupanga ustawi wa mji lakini
imeshindwa kufanya hivyo, jambo ambalo linawakera wananchi wa Dodoma na
kusababisha kukichukia Chama Cha Mapinduzi na Serikali yao,” alisema.
Kutokana na
hoja hiyo kushangiliwa na madiwani pamoja na wana CCM na wananchi wengine,
Malole aliendelea kufafanua kuwa suala la kupigania wananchi wapate viwanja
linamuweka katika hali ngumu kwa sababu anatishiwa kuwa hatapata nafasi ya
kugombea ubunge tena.
“Mimi nasema,
ikimpendeza Mungu kuwa mbunge nitaendelea kuwa mbunge na kama siyo mpango wa
Mungu basi, kwani kuna propaganda nyingi juu yangu lakini hiyo yote ni kutokana
na kupigania wananchi wapewe haki zao,” alisema.
Baada Malole
kutoa madai hayo, Lukuvi ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya CDA alilazimika
kupanda jukwaani ili asawazishe kauli za mbunge huyo, jambo ambalo liliibua
zogo na wananchi kuzomea.
Zomeazomea
dhidi ya Lukuvi ilitawala katika kipindi chote alichokuwa jukwaani huku
viongozi wa chama wakihaha kuwazuia wanachama na madiwani wa CCM wasizomee bila
mafanikio.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “LUKUVI AZOMEWA MBELE YA KIKWETE.”
Post a Comment