Friday, September 19, 2014
MAAJABU YA MTOTO WA MIUJIZA, NI YULE ALIYEPANDA NDEGE HADI ZANZIBAR BILA KUJULIKANA, STORI YAKE HII HAPA
Do you like this story?
![]() |
Mtoto Happiness (10) anayedaiwa kuzua kizazaa mjini Zanzibar. |
![]() |
Mtoto Happiness akiwa na mama yake mzazi, Sarah Zefania. |
![]() |
Mtoto Happiness katika pozi. |
MTOTO
Happiness (10) (pichani) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alizua
kizazaa mjini Zanzibar baada ya kuonekana akizungumza na viumbe wa ajabu na
wanyama, ametua jijini Dar kufuatia kufika kisiwani humo kimaajabu.
Kwa
mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Sarah Zefania, mwanaye Happiness alianza
kuonesha maajabu Zenji tangu alipoonekana kwenye uwanja wa ndege kisiwani humo
wiki iliyopita.
Alisema maofisa wa uwanja huo walipigwa butwaa baada ya kumwona mtoto huyo uwanjani amepita sehemu zote za ukaguzi ambazo abiria asiyekaguliwa nyaraka zake za kusafiria na mitambo maalum ya kuangalia vitu mbalimbali vikiwemo kemikali hatari, silaha na madawa ya kulevya hawezi kupita.

Kwa mujibu wa mama
huyo, aliambiwa na maofisa wa uwanja huo kuwa sehemu hizo zote mtoto wake
alipita bila kuonekana na kamera za uwanjani hapo wala kuacha kumbukumbu yoyote
hali iliyozidi kuwaumiza vichwa maofisa wa uwanja huo.
Zefania alisema
wakati maofisa hao wakitafakari hayo, ndipo msamaria mwema mmoja alijitokeza na
kumchukua kwenda kumuhifadhi nyumbani kwake.
“Akiwa
nyumbani kwa msamaria mwema huyo, nimeambiwa mwanangu alianza kumfanyia maajabu
mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wanyama na viumbe wengine wa ajabu au kutoka
nje huku mlango umefungwa kwa ndani.
“Kuna muda alizungumza na viumbe wasioonekana ambapo aliwasiliana nao na kumletea vitu kadhaa alivyovitaka. Wakati mwingine alizungumza na wanyama wa mle ndani, kama kuku na paka ambao alikuwa akiwatuma kumfanyia yote aliyokuwa akiwaagiza.
“Hali hiyo ilimshtua yule msamaria mwema naye aliomba kupambazuke ili ampeleke mwanangu ustawi wa jamii. Yaani nahisi pengine angekuwa amemuokota sehemu bila kukabidhiwa mbele ya mashahidi pengine angemtupa usiku huohuo.
“Baada
ya kushuhudia vituko hivyo, asubuhi iliyofuata alimkimbiza ustawi wa jamii
ambako nako wameniambia alianza kuwafanyia vituko kama hivyo na kuwaambia kuwa
angewatoroka muda wowote, kisha kuonekana akiparamia juu ya paa na kutaka
kutoka.
“Yaani kwa muda mfupi waliokaa naye, maofisa wa ustawi wa jamii wanasema amewahenyesha vya kutosha ndipo walipofanya juhudi za kunitafuta na mimi nikaenda kumfuata,” alisema mama huyo muda mfupi baada ya kutua bandarini Dar.

Paparazi wetu alipomtaka mtoto huyo kuzungumza alikataa katakata na kujifanya bubu hali iliyomshangaza hata mama yake. “Nashangaa, sijui kwa nini hataki kuzungumza na wewe wakati ni mzungumzaji sana,” alisema mama Happiness.
Akizungumzia historia ya mtoto huyo, mama huyo alisema alimzalia Musoma, Mara na mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina la Juli ambaye walitengana na hawana mawasilino mazuri.
Mama
huyo alisema alimpeleka mtoto wake shuleni lakini kila akifika harudi nyumbani
na kutorokea anakokujua na kuonekana baada ya wiki mbili au tatu.
Kufuatia hali hiyo amewaomba wasamaria wema na viongozi wa dini kumwombea mtoto wake ili arudi katika hali ya kawaida kwani anajua kuna mkono wa mtu wa karibu uliyemharibu mtoto wake.
CREDITS:GPL
Kufuatia hali hiyo amewaomba wasamaria wema na viongozi wa dini kumwombea mtoto wake ili arudi katika hali ya kawaida kwani anajua kuna mkono wa mtu wa karibu uliyemharibu mtoto wake.
CREDITS:GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAAJABU YA MTOTO WA MIUJIZA, NI YULE ALIYEPANDA NDEGE HADI ZANZIBAR BILA KUJULIKANA, STORI YAKE HII HAPA ”
Post a Comment