Friday, September 19, 2014
WANAFUNZI HAWA WASHINDA KUTWA NZIMA WAKIFYATUA MATOFALI BILA KUINGIA DARASANI SHINYANGA
Do you like this story?
WAKATI serikali ikiwa
katika utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa, hali imeonekana kuwa
tofauti katika shule ya sekondari Mwantini iliyopo halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga mkoa wa Shinyanga baada ya kukutwa na waandishi wa habari wakifyatua
matofali ya shule
majira ya saa 5:00 asubuhi muda ambao wangetakiwa kuwa darasani wakiendelea na vipindi vya masomo.
majira ya saa 5:00 asubuhi muda ambao wangetakiwa kuwa darasani wakiendelea na vipindi vya masomo.
Wanafunzi hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo wiki nzima bila
kuingia darasani huku wakikosa masomo ambayo ni haki yao ya msingi.
Katika mahojiano na
waandishi wa habari wanafunzi hao walisema wanasikitishwa na kitendo cha
walimu kuwafanyisha kazi hiyo muda wa masomo wakati wengine
wanajiandaa kuanza mitihani ya kidato cha pili na cha nne jambo ambalo linaweza
kusababisha kiwango cha taaluma kushuka na kushindwa kufikia malengo ya matokeo
makubwa sasa(BIG RESULTS NOW BRN).
Kazi
ya kufyatua matofali inaendelea ambapo kwa shule nzima uanzia kidato cha kwanza
wanatakiwa kufyatua matofali 20,000 ,ambayo watayagawa kwa idadi kwa kila
kidato ili kufikia idadi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI HAWA WASHINDA KUTWA NZIMA WAKIFYATUA MATOFALI BILA KUINGIA DARASANI SHINYANGA”
Post a Comment