Tuesday, September 2, 2014

NYOTA WALIOVUNA FEDHA NYINGI USAJILI 2014/15


Shomari Kapombe -Azam FC

Frank Domayo - Azam


Kama ilivyozoeleka katika kila kipindi cha usajili, wapo wachezaji watakaotawala mazungumzo ya wapenzi wa soka kutokana na usajili wao kuzigharimu fedha nyingi klabu zao mpya na wakati mwingine klabu za awali.

Jambo hili hutokea katika ligi za nchi mbalimbali duniani kote zikiwamo zile zenye umaarufu kama vile Ligi Kuu England, Hispania (La Liga) , Italia (Serie A) na Ujerumani (Bundesliga).

Mara zote wachezaji wanaonunuliwa kwa fedha nyingi kipindi cha usajili ni wale walioonyesha viwango vya juu na kuwa tegemeo kwa klabu zao msimu uliotangulia.

Kwa kifupi, kipindi cha usajili ni kipindi cha neema kwa wachezaji binafsi, pia kwa klabu zao zinazowamiliki kutokana na kupata fedha nyingi kulingana na thamani wanayoonyesha ndani ya uwanja.

Kwenye kipindi cha usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaoanza Septemba 20, pia unawakuta wachezaji walioacha historia kwa kuvuna fedha nyingine kupitia mikataba mipya.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji walionunuliwa kwa fedha nyingi na kuacha historia kwenye dirisha la usajili kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2014/15:

Shomari Kapombe -Azam FC (Sh105 milioni)
Beki Shomari Kapombe aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mzalendo aliyesajiliwa kwa fedha nyingi wakati Azam FC ilipomnunua kutoka timu ya daraja la nne ya As Cannes ya Ufaransa.

Inadaiwa kuwa Azam ilimnunua Kapombe ambaye pia ni beki wa zamani wa Simba baada ya ‘kuvunja benki ‘kwa kuipa AS Canes kitita cha Sh 105 milioni.

Awali rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa ambaye mwaka 2010 alihamia Azam kutoka klabu hiyo ya Jangwani kwa dau la Sh 98 milioni.

Frank Domayo - Azam (Sh70 milioni)
Hakuna ubishi kwamba kiungo huyu wa zamani wa Yanga ndiye mchezaji ambaye usajili wake ulijadiliwa zaidi na wapenzi wa soka hasa wa Yanga baada ya kusajiliwa na Azam FC kwa dau la Sh 70 milioni.

0 Responses to “NYOTA WALIOVUNA FEDHA NYINGI USAJILI 2014/15”

Post a Comment

More to Read