Monday, September 15, 2014
TUTENGENEZE KATIBA INAYOLENGA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI WETU KWA MIAKA 50 IJAYO.
Do you like this story?
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba
Mhe. Prof. Mark Mwandosya ameeleza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2055 Tanzania
itakuwa imeachana na umaskini katika nchi ya uchumi wa kwanza endapo kutakuwa
na dhamira ya dhati hususani kuwa kuandika Katiba yenye kuleta nafuu kwa
watanzania kwani kila kitu kwa Waafrika kinawezekana pasipo kuwa na Wazungu.
Prof. Mwandosya alisema hayo
jana wakati akichangia mjadala wa katiba ndani ya Bunge Maalum, ambapo
alisisitiza umuhimu wa kuwa na katiba itakayozingatia vipaumbele ambavyo
vinaweza kumkwamua mwananchi wa kawaida kuondokana na umasikini na kuliinua
Taifa kiuchumi.
Mhe. Mwandosya amesema kuwa
kuhusu changamoto na kero zinazohusu mambo ya Muungano, katiba imejaribu
kuzizingatia karibia zote, huku akieleza kuwa hali ya Muungano ni imara na
itaendelea kuwa imara.
Ili kufanikisha nchi inapiga
hatua baada ya kuwa na Katiba bora, Mhe. Mwandosya amefafanua kuwa, watumishi
wote wa Umma hawana budi kuliletea tija Taifa hili kwa kuwa misingi imewekwa
ndani ya rasimu ya katiba na kusisitiza kuwa Mtumishi wa Umma sio mtawala
na mambo yanayohusu miiko na maadili ya mtumishi huyo yenye kumtumikia
mwananchi serikali Katiba imeweza kuyazungumzia.
“Tumezungumzia kuhusu rushwa
ambaye ni adui wa haki, kwamba hili tulitambue katika Katiba ili katika Sheria
likasimamiwe vilivyo na pia tumezungumzia pia wale wanaouhujumu uchumi”,
alisema Mhe. Mwandosya.
Kuhusu haki za vijana, Mhe.
Mwandosya ameeleza kuwa katika Rasimu ya Katiba wamezungumzia juu ya haki za
vijana, haki za walemavu, haki za wazee, pamoja na haki za watoto, huku
akiwashangaa baadhi ya wajumbe walioko nje ya bunge hilo wanapotoa shutuma kuwa
wanapoteza wakati kana kwamba hawazungumzii mambo yanayowahusu wananchi.
“Nawaomba wananchi
watusikilize na wayazingatie haya tunayoyasema”. Alisema Mhe. Mwandosya.
Akizungumzia kuhusu Vyombo
vya Usalama, amesema kuwa Katiba inawalinda na kuwatambua viongozi wa usalama,
ambapo sheria inawapa haki hata baada ya kustaafu ili wakaweze kuishi maisha
bora kwa kuchukua dhamana kubwa, hivyo kwa dhamana hiyo viongozi hao
wanapostaafu wanatakiwa kujiepusha na masuala ya kisiasa kwasababu.
“Usalama wa Taifa, Jeshi,
Polisi, Magereza na Uhamiaji, hawa tunawatengezea mambo mazuri sana
wanapostaafu, kwahiyo tafadhari sana mkishatoka tusaidieni, toeni ushauri
lakini mkijiingiza katika siasa na mafaili yetu huku mmeyashika hamtutendei
haki”, alisema Mhe. Mwandosya.
Aidha, ameomba kuwepo na
Randama kwani hiyo inaandikwa katika lugha ambayo mwananchi anaweza kuisoma
tofauti na katiba kwani hiyo inaandikwa kwa lugha ya kisheria, kwahiyo
amependekezo kuwepo na randama kwa ajili ya wananchi.
Mwandosya ameongezea juu ya
suala la amani kuwa ni jambo kubwa sana, amewananga watu wenye tabia ya kutaka
wananchi kuandamana wakapigwe risasi hao ni watu wasioitakia mema nchi, hivyo
amewaasa wananchi walipinge kwa nguvu zao zote kuhusu suala hilo.
“Nina ushauri kwa viongozi
wenye kutaka wananchi wakapigwe risasi na Polisi, naomba watangulie wao
wajipige risasi, unapotaka kuwa Shujaa anzia kwanza wewe mwenyewe, usiwapeleke
vijana ambao ni matumaini ya nchi yetu, ndugu zangu hili jambo siyo la busara
hata kidogo na wananchi mnapokwenda kuandamana, vijana mseme mnaandamana kwa nini?
Kwasababu gani? Na kwa misingi gani na kwasababu ya nani? Ukishajibu haya
maswali kwakweli mtaona nchi yetu kuwa ni nzuri sana, nchi ya amani”,
alisisitiza Mhe. Mwandosya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TUTENGENEZE KATIBA INAYOLENGA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI WETU KWA MIAKA 50 IJAYO.”
Post a Comment