Monday, September 15, 2014
OSCAR PISTORIUS ATACHOMOKA OKTOBA?
Do you like this story?
Pistorius amepewa
dhamana na Jaji Masipa hadi Oktoba 13, hukumu yake itakapotolewa na yuko
hatarini kufungwa miaka 15 jela kwa kuua bila kukusudia, na miaka mitano kwa
matumizi mabaya ya bastola mgahawani.
Familia ya marehemu
Reeva Steenkamp, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na mwanariadha mwenye
ulemavu raia wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imekasirishwa na uamuzi wa jaji
wa kesi hiyo iliyotikisa dunia.
Jaji anayeendesha
kesi hiyo, Thokozile Masipa, alimfutia Pistorius hatia ya kuua kwa kukusudia,
hivyo kumkuta na hatia ya mauaji ya kutokusudia, sambamba na hatia nyingine ya
matumizi mabaya ya bastola akiwa mgahawani.
Pistorius amepewa
dhamana na Jaji Masipa hadi Oktoba 13 hukumu yake itakapotolewa na yuko
hatarini kufungwa miaka 15 jela kwa kuua bila kukusudia, na miaka mitano kwa
matumizi mabaya ya bastola mgahawani.
Hatia hizo,
zimemsukuma mama wa Reeva, June Steenkamp kusema kuwa mwanawe ambaye alikufa
vibaya hakufanyiwa haki katika mfululizo wa kesi hiyo, kwa kitendo cha kumfutia
mashitaka ya kuua kwa makusudi.
June amesema kuwa,
hakuamini kwamba Jaji Masipa alikubali ushahidi wa Pistorius, kwamba aliftaua
risasi bafuni akidhani kuwa alivamiwa na majambazi na hakujua kuwa ni Reeva
ndiye aliyekuwa ndani ya bafu ya nyumba yao.
Hata hivyo, mjomba
yake Pistorius, alimshukuru Jaji Masipa kwa kumuondolea mashtaka ya mauaji ya
kukusudia mwanariadha huyo maarufu barani Afrika.
Pistorius ataendelea
kuwa nje kwa dhamana hadi Oktoba 13, hukumu yake itakapotolewa, huku familia
hiyo ya Steenkamp ikiona haikutendewa haki bila kujali hukumu atakayopewa baada
ya kuondolewa shitaka la kuua kwa makusudi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ OSCAR PISTORIUS ATACHOMOKA OKTOBA? ”
Post a Comment