Thursday, June 5, 2014
KILA MTANZANIA SASA ANADAIWA SH 6000,000.
Do you like this story?
![]() |
Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia |
Wakati
Serikali ikibanwa na wabunge kwa kushindwa kutekeleza Bajeti ya mwaka 2013/14
kutokana na kutegemea fedha za wahisani, Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na
Biashara imesema deni la taifa limeongezeka kwa Sh8.2 trilioni kwa kipindi cha
miezi saba tu.
Ilisema
jana kuwa hadi Juni, mwaka jana deni hilo lilikuwa Sh21.2 trilioni lakini hadi
Januari mwaka huu, deni hilo lilipaa hadi Sh29.4 trilioni na fedha hizo
zimekopwa kwa ajili ya kuendeshea warsha, semina, safari, mafunzo na
matengenezo ya magari.
Akiwasilisha
taarifa ya kambi ya Upinzani, Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia alisema
ukiligawanya deni hilo kwa idadi ya Watanzania milioni 45, kila mwananchi
atakuwa anadaiwa Sh600,000.
Kati
ya Sh5.8trilioni za bajeti ya Wizara ya Fedha mwaka 2014/15, Sh4.3trilioni
zimetengwa kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa
Akiwasilisha
taarifa ya Kamati, Mwenyekiti wake, Luhaga Mpina alisema Sh24.18trilioni ni
deni la Serikali, Sh3.75trilioni ni deni la sekta binafsi na Sh1.15trilioni ni
deni la Benki Kuu Tanzania (BoT).
“Ongezeko
hili la deni haliendi sambamba na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na
ujenzi wa miundombinu ya uchumi. Hali hii inajenga hofu kuwa huenda deni hili
limekuwa ni uchochoro wa ubadhilifu wa fedha za umma,” amesema Mpina.
Amesema
licha ya Serikali mara kadhaa kueleza kuwa deni hilo ni himilivu, kuna
viashiria vinavyoonyesha kuelemewa kwa taifa na mzigo mkubwa wa madeni.
“Mfano
ni mapato ya ndani yamezidiwa na matumizi ya kawaida hivyo kuifanya Serikali
kukopa hata kwa ajili ya warsha, semina, safari, mafunzo na matengenezo ya
magari,” alisema Mpina.
“Deni
la Taifa sasa limefikia asilimia 47 ya Pato la Taifa na kwa kipimo cha bei ya
sasa deni la taifa limefikia asilimia 24, huku deni la nje pekee likiwa ni
asilimia 19” alisema Mpina na kuongeza:
“Licha
ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kuahidi kwa muda mrefu
kufanya ukaguzi maalumu wa deni la taifa, hadi sasa taarifa yake
haijawasilishwa. Ni lini taarifa hiyo itawasilishwa bungeni ili kuwawezesha
wananchi kufahamu undani wa jambo hili?” alihoji.
Kamati
hiyo pia iliilipua Serikali kwa kuuza mashine za elekroniki (EFD), kati ya
Sh600,000 hadi 700,000 kwa maelezo kuwa kiwango hicho ni kikubwa kwa mzunguko
wa biashara ya mtaji wa Sh14 milioni kwa sababu mtaji wake hauzidi Sh5milioni.
Mpina
alisema mashine hizo zinatakiwa kugawiwa bure kwa wafanyabiashara wenye kipato
chini ya Sh40milioni na kufafanua kuwa chombo hicho chenye taarifa muhimu za
mapato ya Serikali hakitakiwi kuuzwa na kufanyiwa matengenezo na mtu binafsi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KILA MTANZANIA SASA ANADAIWA SH 6000,000.”
Post a Comment