Monday, September 15, 2014
WAATHIRIKA WA MABOMU YA MBAGALA WALIA KWA KULIPWA FIDIA KIDUCHU.
Do you like this story?
ZAIDI ya waathirika 1,000 milipuko ya mabomu Mbagala,
wameomba Serikali kuingilia kati na kuwasaidia, ili wapate fidia inayostahili
kutokana na mali na vitu vyao vilivyoharibiwa wakati wa mlipuko huo Aprili
2009.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana
mbele ya baadhi ya waathirika hao, Katibu wa Kamati ya Waathirika hao, Thomas
Mbasha, alisema baada ya ajali hiyo, walilipwa fidia ndogo na waliandika
malalamiko yao kwa njia ya maandishi kwa Serikali wakitaka kuongezwa fidia,
lakini hawajapata majibu mazuri.
“Tumeandika
barua kadhaa kwa Serikali tukiomba fidia zetu lakini hakuna kilichofanyika.
Tunahitaji Rais aingilie kati suala hili ili tulipwe stahili zetu kabla
hajaondoka madarakani,” alisema.
Mbasha alisema fidia walizolipwa awali, hazikulingana na
thamani ya mali na vitu walivyopoteza wakati wa mabomu hayo.
“Inakatisha
tamaa kusema haya mbele ya umma lakini ndicho tulichopewa na Sserikali kama
fidia,” alisema huku akionesha nakala za hundi zikiwa na kiasi
walicholipwa.
Baadhi ya hundi za malipo hayo kutoka Benki Kuu (BoT)
zilikuwa za Sh 1,400; Sh 2,700; Sh 1,950 na Sh 4,900.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stephen Gimonge alisema Rais
Kikwete alitembelea eneo hilo na kuahidi kuhakikisha waathirika wanalipwa fidia
inayostahili lakini ahadi hiyo haijazaa matunda.
Wakizungumza na waandishi wa habari, waathirika hao
waliokuwa wamekusanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mbagala Kuu,
wilayani Temeke walithibitisha kupokea hundi zenye kiasi kidogo cha malipo ya
fidia, huku wengine wakiandikiwa kulipwa Sh 1,000.
Omary Mbonde ambaye ni mmoja wa waathirika hao,
alithibitisha kulipwa hundi ya fidia ya Sh 1,950.
“Fedha
hizo nimelipwa kama fidia kwa ajili ya nyumba yangu iliyoharibika pamoja na
vitu vyangu vingine,” alisema na kuongeza kuwa alipeleka malalamiko yake kwenye
kamati, ili apate fidia inayostahili lakini hadi leo hajapata chochote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAATHIRIKA WA MABOMU YA MBAGALA WALIA KWA KULIPWA FIDIA KIDUCHU.”
Post a Comment