Tuesday, October 7, 2014
KIJANA AZIMIA BAADA YA KUCHAPWA VIBOKO 120 MKOANI ARUSHA
Do you like this story?
SHERIA iliyopitishwa na wakazi wa Arumeru
mkoani Arusha ya kuwachapa viboko 70 hadi 120 wasichana wanaovaa nusu uchi na
wavulana wanaovaa mlegezo, kuvuta bangi, wizi, matusi na ulevi nyakati za kazi
imeanza kufanya kazi baada ya kijana Zakayo Leonard (26) kuchapwa viboko 120
kwa makosa mbalimbali likiwemo uchafu wa kutofua nguo zake.
Kijana huyo mkazi wa
Ilboru, alihukumiwa adhabu hiyo kwa kuchapwa viboko 70 akidaiwa kutenda
kosa la kumshambulia baba yake mzazi aliyetambulika kwa jina la
mzee Ng’uraa na kumng’oa jino moja.
Pia alitandikwa
viboko 30 kwa kosa la kumtolea maneno machafu mzee wa kimila (Laigwanani) na
baadaye alicharazwa viboko 20 kutokana na tabia ya uchafu wa kutofua nguo zake.
Hata hivyo, mara
baada ya adhabu hiyo ya viboko 120 kwa mkupuo, kijana huyo alizimia na
kushindwa kuinuka wala kutembea hali iliyolazimika kusaidiwa kwa kubebwa na
morani wa Kimasai hadi nyumbani kwake.
Adhabu hiyo
ilitekelezwa hadharani mbele ya wazee wawili wa ukoo (Laigwanani) waliokuwa
wakishuhudia huku mtuhumiwa akitakiwa kutojigusa popote wakati wa utekelezaji
wa adhabu hiyo na kwamba iwapo angejishika popote viboko hivyo alivyochapwa
vingefutwa na kurejea upya.
Wazee wa makabila ya
Wamasi, Waarusha na Wameru wamejiwekea utaratibu wa kimila bila kujali kama
unafuata maadili ya mwanadamu kwa kuwaadhibu wahalifu hadharani bila
kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
credits:gpl
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)



0 Responses to “KIJANA AZIMIA BAADA YA KUCHAPWA VIBOKO 120 MKOANI ARUSHA ”
Post a Comment