Tuesday, October 7, 2014
MKURUGENZI WA TFF ATUPWA JELA MIAKA SITA, NI ELLIUD MVELLA MAARUFU KWA JINA LA MAHANJI.
Do you like this story?
| Mvella mwenye suti ya michezo siku moja kabla hajahukumiwa |
MAHAKAMA ya Mkoa ya
Iringa jana imemtia hatiani Mkurugenzi wa Sheria na Utawala wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Eliud Mvella baada ya kupatikana na makosa
manne ya kuendesha biashara ya bima bila kibali.
Mvella aliyewahi kuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi Mkoa wa Iringa kabla ya kutimkia CCM
katika miaka ya karibuni na kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) alihukumia miaka sita au kulipa faini ya Sh Milioni 3 baada ya
kupatikana na hatia ya kutenda makosa hayo.
Mvella aliyewahi kuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) alikwepa
kutumikia kifungo cha miaka sita jela baada ya kufanikiwa kulipa faini ya Sh
Milioni 3 iliyolipwa kupitia risiti namba 3425607.
Mvella ambaye mjini
hapa anajulikana zaidi kwa jina la Mahanji alifikishwa katika mahakama hiyo
akituhumiwa kwa kosa la kwanza la kuendesha biashara ya bima bila kibali, pili
kufanya shughuli za bima bila usajiri, tatu kuuza stika za bima za magari na
kava noti bila kibali na nne kutoa risiti za bima bila kibali.
Akitoa hukumu hiyo,
Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Ruth Massam alisema
Mahanji alitenda makosa hayo Mei 25, 2013 katika jengo la Higlands hall kwa
kutumia kampuni ya bima hewa iliyojulikana kama Emock.
Alisema katika kosa
la kwanza, mahakama hiyo imemtia hatiani Mvella na imempa adhabu ya kifungo cha
miaka miwili gerezani au faini ya Sh Milioni moja.
Kwa mujibu wa hakimu
huyo, Mvella amehukumiwa miaka miwili gerezani au faini ya Shmilioni moja kwa
kosa la pili na kifungo cha miaka miwili au faini ya Sh Milioni moja kwa kosa
la tatu na nne.
Kwa kupitia kampuni
hewa ya bima ya Emock, Mvella alitenda makosa hayo kwa kutumia kampuni ya Bima
ya Mwananchi yenye makao yake makuu Arusha wakati hakuwa mwajiliwa wa kampuni
hiyo.
Alisema mshakiwa
alikutwa na vifaa vya kampuni hiyo kwenye ofisi iliyopo jengo hilo la Highland.
Hata hivyo ofisi hiyo
haikuwa na kibao cha jina la kampuni lakini risiti zake zilikuwa
zikionesha kuwa inafanya kazi za Kampuni ya Bima ya Mwananchi.
Alisema Mvella
alikuwa amewaajiri wanawake wawili kwa ajili ya utoaji wa huduma hizo za bima
kwa kupitia kampuni hiyo hewa ya Emock.
Wakili wa Serikali
Alex Mwita aliiomba Mahakama hiyo iangalie namna ya kumpunguzia adhabu
mshitakiwa huyo kwa kuwa hajawahi kutenda kosa lolote.
Hakimu alitoa fursa
kwa wakili wa utetezi, Erick Nyato ambaye alimwachia mshitakiwa ajitetee
mwenyewe.
Mvella alisema
anaomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kuwa na ndugu wanaomtegemea
akiwemo mama yake mzazi ambaye ana umri mkubwa na watoto wanaosoma shule na
vyuo.
Alisema pia anafanya
kazi za kijamii kupitia shirika la IYODEA (Iringa Youth Development
Association).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)

0 Responses to “MKURUGENZI WA TFF ATUPWA JELA MIAKA SITA, NI ELLIUD MVELLA MAARUFU KWA JINA LA MAHANJI.”
Post a Comment