Saturday, November 22, 2014
AFARIKI DUNIA BAADA YA NDEGE KUKATAA KUMSAFIRISHA ILI AKATIBIWE
Do you like this story?
Sande
Jacob Mremi amefariki Siku chache baada ya kukosa usafiri wa ndege ambapo
alitakiwa kwenda nje ya nchi kupata matibabu.
Kituo cha ITV kiliripoti kuhusu habari za kijana huyo kuumwa na kutokana na kusumbuliwa tatizo la uzito mkubwa nakushindwa kupata Ndege ya kumsafirisha kwenda kwenye matibabu India kijana huyo amefariki Dunia.
Ndugu wa kijana huyo walilalamika kutoridhishwa na baadhi ya Mashirika ya Ndege kwa kushindwa kuwasaidia kumsafirisha ndugu yao.
Katika mahojiano na ITV mama wa mtu huyo amesema; “..yaani kwa kweli mashirika ya Ndege hayakuweza kutufanyia haki kwa kweli, wametunyanyasa kwa sababu tulipokuwa tunapeleka maombi tunataka kumsafirisha mtoto wetu ilikuwa wao watusaidie na kutupa maelekezo tunatakiwa tufanye nini na nini, lakini baada ya kuona tunakosa msaada ndio tukaamua kuja ITV ili watusaidie, kwa hiyo yeye mwenyewe akaanza kupata presha kwa sababu presha alikuwa hana mpaka anapanga kusafiri alikuwa hana presha nilimpima vipimo vyote alikuwa hana tatizo lolote…”
Dada wa marehemu amesema; “..Ethiopia walitusaidia kwa kweli mpaka hatua ya mwisho na Jumapili kama Mungu angemuweka hai Ethiopia wangemsafirisha, na mashirika ya Ndege mengine yalitakiwa yatuelekeze hivi, lakini sasa kutokana na ile hali mara leo kapelekwa kesho anarudishwa mdogo wangu kesho kutwa kapelekwa amerudishwa mdogo wangu, msongo wa mawazo umemkaa rohoni anashindwa kuongea maskini ya Mungu, mawazo mpaka yamemfanya mdogo wangu afariki baada ya kupatwa na presha.

Baba
wa Sande amesema; “…wakatumia sheria ya pili ya kunihusisha mimi wakaniambia
bwana kumbe mtu huyu ni mkubwa sana tunatakiwa tuvunje viti tumbebe,
nikawauliza nikulipeni bei gani? wakaniambia tulipe dola elfu saba mia tano na
thelathini na nne, na mara ya kwanza tulilipa dola elfu sita miambili
ishirini…”
Bado haijafahamika kama Shirika hilo la ndege litarudisha hela ambayo ililipwa na watu hao kwa ajili ya kumsafirisha ndugu yao.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ AFARIKI DUNIA BAADA YA NDEGE KUKATAA KUMSAFIRISHA ILI AKATIBIWE ”
Post a Comment