Tuesday, November 18, 2014

SERIKALI WILAYANI KAHAMA YAOMBWA KUPAMBANA NA WIMBI LA VIJANA WANAOVUTA BANGI.




SERIKALI Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imeombwa kuingilia kati na kupiga marufuku wimbi la vijana waliochini 18 wanaojihusisha na uvutaji wa bangi na madawa ya kulevya ambao wamekuwa tishio kubwa  katika jamii.

Wito huo umetolewa leo na kiongozi wa Mtaa wa Majengo ya Kefulatino Wilayani Kahama,Selemani Juma wakati akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi  ambapo amesema zaidi ya vijana 100 walivamia nyumba moja mtaani kwake na nakufanya uhalifu wa vitu mbalimbali ikiwemo kuiba nguo za familia zilizoanikwa.

Amesema kuna vurugu kubwa ilitokea juzi majira ya saa tano asubuhi ambapo kundi kubwa kutoka Nyihogo lililojitambulisha kwa jina la USWAZ CAMP lilikwenda majengo kwa lengo la kuwatafuta vijana wa kikundi  cha majengo kinachojulikana kwa jina SKL.

Kwa mujibu wa Juma amesema vijana wa Uswazi Camp kikundi cha Nyihogo walivamia mtaa wake kwa lengo la kuwatafuta vijana wa kikundi cha SKL cha Majengo ambao walimjeruhi kijana wa USWAZI CAMP pia walifika mtaani kwake wakiwa na siraha mbalimbali kama mapanga,mundu,moko,mafyekeo,pamoja na viboko.

Katika hatua nyingine Juma amelitupia lawama jeshi la Polisi wilayani humo kutofika kwa wakati kipindi wanapojulishwa na wanapopigiwa simu yao ya dharula kutopokelewa haraka kitendo ambacho kinachelewesha na huenda kinahatarisha amani.

Amesema zaidi kikundi hicho cha vijana wa majengo sokola (SKL )wamekuwa ni tishio mitaani ambapo viongoz a mitaa wamekuwa wakiitisha mikutano mbalimbali na wazazi wao kuzungumzia hali hiyo lakini hakuna mwitikio wowote hivyo wazazi ndiyo wanachangia kwa kiasi kikubwa.

Amesema matukio mengi ya uhalifu yanayotokea katika mitaa yao yanasababishwa na uzembe wa Jeshi la Polisi pamoja na Mapolisi kata  kutowajibika ipasavyo katika kitengo chao hivyo ameiomba Serikali kulivalia njuga suala hilo ili kuwanusuru raia wema na mali zao.

0 Responses to “SERIKALI WILAYANI KAHAMA YAOMBWA KUPAMBANA NA WIMBI LA VIJANA WANAOVUTA BANGI.”

Post a Comment

More to Read