Tuesday, November 18, 2014
UMEIPATA HII KUHUSU ULINZI WA SERIKALI DHIDI YA JAJI WARIOBA? SOMA HII
Do you like this story?
Ni siku kumi na tano zimepita tangu
kuripotiwa tukio la vurugu katika mdahalo wa Katiba uliohudhuriwa pia na
aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba Katiba
Novemba 2 2014, jana katika Kikao cha Bunge Dodoma ishu ya walinzi kama wazee
kama Warioba imechukua headlines kwenye maswali na majibu.
Akiuliza swali hilo Mbunge Moses
Machali amesema; “…Majuzi hapa Mzee Warioba tunaelewa wote hapa Wabunge kwamba
amefanywa nini pale Ubungo Blue Pearl Hotel.. Na hapo kwenye swali la msingi la
Mheshimiwa Selasini limezungumzia suala la ulinzi kama umeliangalia swali hili,
sasa waziri unaposimama na kulieleza Bunge kwamba wazee hawa wanajaliwa vizuri,
mambo ya usalama yako sawasawa ni kutowatendea haki wazee hawa…”
“…Mawaziri ambao wanatoa majibu ya
namna hii tunawafanya nini kwa sababu wanazungumza uongo ambao uko wazi, hili
jambo ni suala la juzi.. Vinginevyo Mheshimiwa Kombani aombe radhi katika suala
hili…”– Machali
Akijibu swali hilo Celina Kombani
amesema “… Mimi ndiye Waziri ninayewatunza wazee, na ninachokisema nina uhakika
nacho… Mzee Warioba anapata ulinzi kama walivyo wazee wengine.. na mfano
mzuri mnamuona Mheshimiwa Lowassa hapa anapata ulinzi, Mheshimiwa Shamsi Vuai anapata
ulinzi…”
“…Kwa
hiyo wazee wastaafu wote wanapata ulinzi.. Unless kama ameacha walinzi wake…
Nna uhakika na ninachosema analelewa, anatunzwa na ukitaka ushahidi nenda
kamulize kama hapati facilities zote zinazostahili kwa viongozi wastaafu…”–
Kombani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UMEIPATA HII KUHUSU ULINZI WA SERIKALI DHIDI YA JAJI WARIOBA? SOMA HII ”
Post a Comment