Wednesday, December 17, 2014
HOSPITALI YA APOLLO YAFANIKIWA KUTENGANISHA MAPACHA KUTOKA TANZANIA WALIOUNGANA.
Do you like this story?
December 16, 2014: Watanzania waendelea kufaidika kutoka kwa hospitali ya
Apollo iliyoko nchini India. Hii ni kufuatia hosiptali hiyo kufanikiwa
kuwatenganisha mapacha wa kike Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini
ya kifua na tumboni kutoka nchini Tanzania katika upasuaji uliofanyika tarehe
17 Novemba 2014 nchini India. Mapacha waliounganika kwa mtindo huu hujulikana
kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji uliofanyika na hospitali
Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.
Mapacha Abriana na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika
kuanzia chini ya kifua na tumbo, hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja
wa moyo na maini yaliyounganika. Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa
kwa madaktari ulikuwa kufanya utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi ambayo
waliweza kukabiliana nayo ipasavyo kutokana na madaktari waliokuwepo wenye
wataalum wa kiufundi na matibabu.
Upasuaji huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma
mbali mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa
masaa 11. Watalaamu walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyo kuwa
vimeungana lakini mapacha hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo
kusaidia zoezi zima la uponyaji baada ya upasuaji.
Hali kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa
kurudisha viungi husika katika mahala pake baada ya kuvitenganisha.
Akizungumzia kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive
Surgeon anasema, “Baada ya upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa
kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini
yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa nne
kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahala pake.”
Upasuaji huu wa mafanikio wa mapacha waliounganika kutoka ncini Tanzania
sio wa kwanza kufanywa na hospitali ya Apollo. Mwishoni mwa mwaka 2013 mapacha
wengine wakiume waliokuwa wameungana na kujulikana na wataalamu kama Pygopagus,
Ericana & Eluidi kutoka Tanzania walifanikiwa kutenganishwa na wataalamu wa
hospitali hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HOSPITALI YA APOLLO YAFANIKIWA KUTENGANISHA MAPACHA KUTOKA TANZANIA WALIOUNGANA.”
Post a Comment