Wednesday, December 17, 2014
WAKURUGEZI WATANO WASIMAMISHWA KAZI KATIKA SAKATA LA UCHAGUZI
Do you like this story?
Serikali imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita wa Halmashauri, na
kuwasimamisha kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana na kubainika
kuchangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14,
mwezi huu.
Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika
katika uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema uamuzi huo pia umeridhiwa
na Rais Jakaya Kikwete.
Mhe. Ghasia amewataja halmashauri ambazo wakurugenzi hao waliotenguliwa
uteuzi wao kuwa ni za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda,
waliosimamishwa kazi ni wakurugenzi wa Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na
wa Manispaa ya Sumbawanga.
Waziri Ghasia amesema kuwa Wakurugenzi wengine watatu wapewa onyo kali,
ambao ni wa Rombo, Busege na Muheza na wengine watatu wakipewa onyo la kawaida,
wakurugenzi hao ni wa Manispaa Ilala, Hai na Mvomero.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAKURUGEZI WATANO WASIMAMISHWA KAZI KATIKA SAKATA LA UCHAGUZI ”
Post a Comment