Tuesday, December 16, 2014

NAIBU WAZIRI AVAMIWA NA VIBAKA NA KUPORWA WAKATI AKIENDA ZAHANATI KUTIBIWA




Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga mjini amevamiwa na kundi la vibaka wakati akienda Zahanati kupatiwa matibabu na kisha kuporwa vitu mbalimbali mjini Shinyanga.

Masele alisema tukio hilo lilitokea juzi saa4 usiku wakati akienda kupatiwa matibabu ya matatizo ya koo katika Zahanati ya Bakwata  na gafla alivamiwa na kundi la watu wapatao 30 na kumpora mali zake.

Alisema akiwa na Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar,Vuai Aly wakipata chakula cha usiku hotelini gafla alijisikia vibaya na kuamua kwenda kwenye Zahanati hiyo kupatiwa matibabu na ndipo alipata mkasa huo wakati akiwa njiani.

Masele alikanusha tuhuma alizozushiwa na wananchi kuwa kuporwa huko kunatokana na yeye kugawa rushwa kwa wananchi wakati wa kampeni Serikali za mitaa ili wananchi wawachague wagombea wa CCM.

0 Responses to “NAIBU WAZIRI AVAMIWA NA VIBAKA NA KUPORWA WAKATI AKIENDA ZAHANATI KUTIBIWA ”

Post a Comment

More to Read