Wednesday, December 17, 2014

NEWS ALERT: MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JAJI WEREMA AJIVUA GAMBA KUTOKANA NA KASHFA YA ESCROW




Wiki chache zilizopita wakati Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiendelea, macho ya watu wengi na masikio yalikuwa na hamu ya kutaka kuujua mwisho wa sakata la Escrow.

Wakati watu wengi wakisubiri maamuzi yatakayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuhusiana na Ripoti juu ya issue ya ubadhilifu wa fedha kwenye akaunti ya Escrow, leo December 16 kuna taarifa iliyotufikia muda mfupi iliopita kuhusu kiongozi mmoja wa Serikali kujiuzulu.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

0 Responses to “ NEWS ALERT: MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JAJI WEREMA AJIVUA GAMBA KUTOKANA NA KASHFA YA ESCROW ”

Post a Comment

More to Read