Tuesday, December 16, 2014
TANZANIA YAENDELEA VEMA NA MPANGO WA KUTOA ELIMU YA MSINGI
Do you like this story?
Na Eleuteri Mangi- Arusha.
Serikali ya
Tanzania inaendelea vema na mpango wake wa kutoa elimu ya msingi kwa watoto
wote waliofikia umri wa kwenda shule nchini.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa wakati
akiwasilisha mada yake inayohusu “Namna Tanzania inavyoboresha Usawa wa Kinga
ya Jamii katika sekta ya elimu” katika kongamano la kimataifa linaloendelea
katika siku ya pili jijini Arusha kuhusu Kinga ya Jamii.
Dkt. Kawambwa
alisema kuwa mpango huo unaanzia elimu ya awali, shule ya msingi na sekondari
ambapo kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule apate elimu ambayo ndiyo msingi
wa kinga ya jamii nchini tofauti na awali ambapo elimu ya msingi ilikuwa kwa
watoto wenye umri kuanzia miaka 7 hadi 14.
Dkt. Kawambwa
alisisitiza kuwa mpango huo wa kinga ya jamii nchini unaenda sanjari na Mpango
wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao Tanzania imeanza kuutekeleza mwezi Aprili,
2013 ambapo unatarajiwa kuhitimishwa 2017.
Ili kufikia
malengo ya kuboresha mpango wa kinga ya jamii nchini, Dkt. Kawambwa aliwaambia
wajumbe wa kongamano hilo kuwa mbinu zinazotumiwa na Tanzania katika kutekeleza
mpango wa BRN na kuboresha kinga ya jamii ni pamoja na kuboresha vifaa vya
kujifunza na kufundishia shuleni, kusimamamia mpango wa wanafunzi kujua kusoma,
kuandika na kuhesabu na kuboresha ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya ndani
na ya taifa.
Mbinu
nyingine ni kuwapa motisha walimu, kutoa motisha kwa shule zilizofanya
vizuri katika mitihani ya taifa kwa shule zote iwe ya msingi au sekondari na
kuwawezesha walimu na wanafunzi kujua wajibu wao kwenye sekta ya elimu ili
kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa ufanisi ili kuongeza nguvu kazi ya wataalam
ambao ndio msingi wa kuboresha kinga ya jamii na hivyo kupunguza tatizo la
umaskini nchini.
Aidha, Dkt.
Kawambwa alisema kuwa viashiri ambavyo vinaonesha Tanzania inaendelea kupata
mafanikio katika kuimarisha sekta ya elimu na kuimarisha kinga ya jamiina ni
pamoja na kuongezeka ufaulu katika mitihani ya taifa ambapo mwa 2013 ufaulu kwa
shule za msingi na sekondari ulikuwa zaidi ya asilimia 60, mwaka 2014 kwa
asilimia zaidi ya 70 na inatarajiwa 2015 ufaulu huo utaongezeka kufikia
asilimia 80.
Akijibu swali
la Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Huduma Ali N.
Ismail kutoka Kenya aliyetaka kujua kwanini Tanzania bado inatumia mpango wa
kupanga shule katika madaraja ambao unaweza kupunguza morali kwa baadhi za
shule ambazo inaweza kuwa chanzo cha kupunguza uwezekano wa kutoboresha
mpango wa Kinga ya jamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TANZANIA YAENDELEA VEMA NA MPANGO WA KUTOA ELIMU YA MSINGI ”
Post a Comment