Thursday, January 8, 2015
BONGO MOVIE KUPAMBA UZINDUZI WA KITABU CHA MAREHEMU KANUMBA LANDMARK HOTEL
Do you like this story?
UZINDUZI wa
kitabu cha msanii wa filamu hayati Steven Kanumba unatarajia kuandika historia
kufuatia maandalizi yaliyopangwa anasema mratibu wa tamasha hilo Mohamed
Mwikongi ‘Frank’ amesema kuwa kutakuwa na mambo muhimu sana kwa ajili ya
kumuenzi msanii huyo ambaye aliitangaza Tanzania kimataifa.
“Tumepanga
kufanya mambo makubwa kwa ajili ya mwenzetu na tunataka ijengeke tabia ya
kuenzi wasanii mbalimbali, pesa za uzinduzi wa kitabu hiki utafungua Kanumba
Foundation kwa ajili ya kusaidia wanawake wajane na watoto yatima,”anasema
Frank.
Frank
anawakaribisha wadau wa Kanumba kwa kufika na kujione kazi za marehemu Kanumba
na kuoshuhudia wimbo maalumu wa Marehemu Kanumba utakaoimbwa na mwanamuziki
nyota Christian Bella kwa ajili ya tukio maalum .
Kitabu cha
historia ya maisha ya mwigizaji nyota Swahilihood Hayati Steven Kanumba
kinatarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 January 2014 katika ukumbi wa Landmark
Ubungo, uzinduzi huo utaambatana na maonyesho ya kazi za marehemu Kanumba
alizowahi kushiriki na kuzifanya.
Mama yake
mzazi akiongea na waandishi wa habari amewashukru wale wote ambao wamekuwa
wakijaribu kufanya kazi ambazo kwa njia moja au nyingine zinamkumbuka mwanaye
ambaye aling’ara katika tasnia ya filamu Swahilihood na kufanikiwa kutangaza
Tanzania.
“Nawashukru
sana watanzania na wale ambao si Watanzania wamekuwa faraja sana kwangu, hasa
pale ambapo wamekuwa wakiona umuhimu wa kumuenzi Kanumba kwa njia tofauti
tofauti, nawashukru sana, na najua kila mtu ana mchango mkubwa si rahisi
kuwataja majina maana mpo wengi,”anasema mama Kanumba.
Kitabu hiki
kinachohusu maisha ya Kanumba The Great Fallen Tree kimeandikwa na E. Emmanuel
kutoka nchini Canada na kuhaririwa nchini Marekani na kufanyiwa uchapishaji
nchini Kenya.
Uzinduzi wa
kitabu utasindikizwa na Christian Bella na Bendi ya Malaika kiingilio ni Ths.
20,000/ na utapata kitabu kimoja bure ukiingia tu mlangoni na kazi zote
za Hayati Kanumba zitapatikana siku hiyo. USIKOSE TUKIO HILI LA AINA YAKE!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BONGO MOVIE KUPAMBA UZINDUZI WA KITABU CHA MAREHEMU KANUMBA LANDMARK HOTEL”
Post a Comment