Thursday, January 8, 2015
DKT. MAGUFULI AAGIZA KUFUNGWA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI KATIKA VIVUKO VYOTE NCHINI.
Do you like this story?
Mfanyakazi wa kivuko cha Kigongo -busisi mkoani Mwanza akionesha wananchi namna ya kutumia mashine hiyo. |
WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ameagiza kufungwa kwa mfumo
mpya wa kielektroniki katika vivuko vyote nchini ili kukabiana na wajanja
wachache wanahujumu mapato katika vivuko hivyo.
Mbali ya hilo, ameagiza kufanywa kwa utaratibu utakaowezesha huduma
katika vivuko zinatolewa kwa saa 24 ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Dkt. Magufuli alitoa maagizo hayo jana katika uzinduzi wa mfumo
mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa
na Kampuni ya Africom Tanzania.
"Tulianze pale Kigamboni na tukaona mafanikio, tulipokuja hapa
(Kigongo) tukaboresha na mafanikio yameonekana kwa kiasi kikubwa. Vivuko vyote
sasa vifungwe mfumo mpya wa kielektroniki.vivuko vyote nchini," aliagiza
Dkt. Magufuli.
Alisema mfumo huo una faida kubwa ikiwemo kudhibiti upotevu wa
mapato ambapo katika kivuko cha kigongo - Busisi alisema mapato yameongezeka
kwa takribani asilimia 40 baada ya kufungwa kwa mfumo huo.
Hata hivyo, Dkt. Magufuli alikataa kutaja ni kwa shilingi ngapi
mapato hayo yameongezeka kwa hofu kuwa watu wenye dhmira mbaya wakisikia
wanaweza kwenda na kufanya uhalifu.
Pia, aliagiza Kivuko kwa Kigamboni nacho kiboreshwe mfumo wake kama
ilivyokuwa kwa Kigongo - Busisi. Waziri huyo wa Ujenzi, alisema kutokana na
mafanikio yanayopatikana katika kudhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha
huduma kwa wananchi, wafanyakazi husika kwa maana ya wale wa TEMESA maslahi yao
yanapaswa kuangaliwa upya na kuboreshwa. "Kama mapato ni mazuri,
wafanyakazi nao walipwe vizuri, wasikae kimasikini kwani wanapaswa kuona mwaka
2015 ni ukombozi katika maisha yao.
Alisema serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete
imefanikiwa kujenga madaraja yote makubwa nchini ambapo kwa sasa kuna madaraja
4880 nchini na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo
yalikuwa ya kuvutwa.
Mfumo wa kielektroniki katika vivuko vya Kigamboni na Kigongo
Busisi ulifungwa na Kampuni ya Africom Tanzania ambaye Mkurugenzi Mtendaji wake
Juma Rajabu alisema watahakikisha wanafunga mifumo ambayo itadhibiti upotevu wa
mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi ambao ndiyo watumiaji.
Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua mfumo mpya wa
kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na
Kampuni ya Africom Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ DKT. MAGUFULI AAGIZA KUFUNGWA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI KATIKA VIVUKO VYOTE NCHINI.”
Post a Comment