Thursday, January 8, 2015

KIJANA ‘AJISALIMISHA’ KUHUSIANA NA SHAMBULIO LA KIGAIDI UFARANSA.


Mtuhumiwa  Cherif Kouachi (kushoto) na ndugu yake Said Kouachi.

Polisi wakiendesha oparesheni ya kuwakamata watuhumiwa katika  kitongoji cha  Croix-Rouge eneo la Reims, kaskazini mwa Ufaransa.

Polisi wakilinda jengo moja huko Reims wakati wapelelezi wakiendesha shughuli zao kuhusiana na shambulio hilo la kigaidi.


NDUGU wawili na kijana mmoja jana walielezewa kuwa ndiyo watuhumiwa watatu wanaohusishwa na shambulio la kigaidi jana dhidi ya jarida lenye kupinga Uislam nchini Ufaransa liitwalo Charlie Hebdo mjini Paris ambapo watu  12 waliuawa na saba kujeruhiwa.

Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na  mhariri mkuu, wachoraji wanne wa vikatuni na polisi wawili.  

Inasemekana sababu ya kuvamiwa kwa ofisi za jarida hilo ni kuchapisha vikatuni vyenye kukashifu dini ya Kiislam.  Washambuliaji hao walitoroka baada ya shambulio hilo.

Watuhumiwa hao ni  Said Kouachi (34), Cherif Kouachi (32) wote wakazi wa jiji la Paris, ambao ni pamoja na Hamyd Mourad (18) kutoka mji wa kaskazini-mashariki wa Reims, Ufarransa, aliyejisalimisha polisi baada ya kuona katika vyombo vya habari alikuwa anatafutwa.

Hivi sasa polisi wanawatafuta ndugu hao wawili katika eneo la Croix Rouge hulo Reims.

0 Responses to “KIJANA ‘AJISALIMISHA’ KUHUSIANA NA SHAMBULIO LA KIGAIDI UFARANSA.”

Post a Comment

More to Read