Wednesday, January 7, 2015

CITY KUWAVAA ‘WAMALAWI’ JUMAMOSI.




Mbeya City  FC  inayoonolewa na Kocha Bora wa msimu uliopita, Juma Mwambusi, Jumamosi Junuari 10  itacheza mechi wa kirafiki dhidi ya Karonga United ya Malawi. mechi ya kirafiki itakayochewzwa wilayani kyela.

Kwa mujibu wa waandaji wa mchezo huo  Chama cha Soka Kyela, kiingilio kimepangwa  kuwa Sh. 1000 ili kuwawezesha  mashabiki wengi kujitokeza kuona mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.

Mwambusi amesema atauchukulia mchezo huu kama kipimo kwa vijana wake  kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar FC utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba Januari 17, kufuatia kuahirishwa kwa michezo yao miwili dhidi ya Simba na Yanga zilizokwenda Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi.

“Ni jambo zuri kupata mechi ya kirafiki ya kimataifa katika wakati huu, tutauchukulia mchezo huu kama kipimo muhimu kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar hasa ukizingatia kuwa Karonga ni timu inashiriki ligi kuu huko Malawi.
"Wote tunafahamu  uwepo wa michauano ya Kombe la Mapinduzi umefanya kuahirishwa kwa michezo yetu miwili iliyokuwa tucheze, hilo halijatuvunja moyo ndiyo maana nasema hiki ni kipimo kizuri tukijiandaa kwenda kucheza mchezo mwingine wa ligi huku lengo letu likiwa ni kupata matokeo mazuri,” amesema Mwambusi.

0 Responses to “ CITY KUWAVAA ‘WAMALAWI’ JUMAMOSI.”

Post a Comment

More to Read