Wednesday, January 7, 2015

TASAF KUTUMIA MIKUTANO YA HADHARA KATIKA MITAA NA VIJIJI KUTAMBUA KAYA MASKINI KATIKA MPANGO WA AWAMU 3.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Abbas Kandoro akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tasaf

Kaimu  Mkurugenzi wa Tasaf Taifa, Zuhura Mdungi  akisoma Taarifa ya utekelezaji.



WAshiriki wa Warsha ya kujenga uelewa kuhusu mpango wa kunusuru kaya maskini kwa viongozi, watendaji na wawezeshaji




Mikutano ya hadhara ya vijiji na mitaa inatarajia kutumika katika kuwatambua walengwa wa mpango wa kuzisaidia kaya masikini unaotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)awamu ya Tatu.
Akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo katika halmashauri ya jiji la Mbeya  mwakilishi wa  mkurugenzi mtendaji wa Tasaf,Zuhura Mdungi alisema kuwa  njia hiyo ya mikutano ya hadhara itasaidia kuwapata walengwa sahihi  wa mpango huo.

Alisema Kuwa katika mikutano hiyo wanakaya wenyewe ndiyo watahusika katika kuwatambua na kuwateua  watu ambao wapo katika kaya masikini waliopo katika maeneo husika ili kuondokana na migongano wakati wa utekelezaji wa mpango huo

Mdungi  alisema  kuwa  malengo ya mpango huo ni kuziwezesha  kaya masikini kuongeza matumizi muhimu kwa njia endelevu,kuwekeza katika rasilimali watu hususani watoto  kwa kuwajenga na kuweza kupata  elimu bora,chakula na kuongeza kipato kwa kupitia uwekaji wa akiba na shughuli za kiuchumi ili kuboresha maisha.

Alisema kuwa mpango huo pia utakuwa unatoa ajira kwa kaya masikini zenye watu wenye uwezo wakufanya kazi wakati wa mjanga mbali mbali kama ukame na mafuriko na kwamba pia mkakati huo umelenga kupunguza mazingira hatarishi kwa kipindi cha kati na kirefu kwa kuwekeza kwewnye elimu,na lishe kwa watoto.

Akizindua mpango huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka viongozi na watendaji kutekeleza mpango huo kwa misingi ya kisiasa kwa kutokuwa na upendeleo katika kutambua kaya masikini.

“Acheni watu watambuane wenyewe na mpango huu usiwe wa kificho wala sisi vbiongozi tusiwe na upendeleo na lisiwe na misingi ya kisiasa hivyo kila mmoja atomize wajibu wake kwa uwazi”alisema

Utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini unatarajia kuzifikia kaya 1milioni zenye watu 7milioni kwa miaka kumi katika awamu mbili za miaka mitano kwa kila awamu.
Mwisho

0 Responses to “TASAF KUTUMIA MIKUTANO YA HADHARA KATIKA MITAA NA VIJIJI KUTAMBUA KAYA MASKINI KATIKA MPANGO WA AWAMU 3.”

Post a Comment

More to Read