Wednesday, January 7, 2015
EWURA YASHUSHA BEI ZA MAFUTA....KUANZIA LEO 7.1.2015
Do you like this story?
Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel (kulia), akizungumza katika mkutano huo. |
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati, Maji na
Mafuta (Ewura), imepunguza bei za mafuta kote nchini kuanzia leo kutokana na
kudorora kwa uchumi wa bara la ulaya.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji
na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini
na katika soko la Dunia.
Alisema
kuanzia leo bei ya mafuta ya petroli kwa lita moja itauzwa sh.1955 na hiyo
inatokana na kushuka kwa jumla ya asilimia 16 sawa na pungufu kwa jumla ya
sh.311 kwa lita.
Alisema
bei ya petroli katika soko la dunia imeshuka kwa jumla ya aasilimia 25 kuanzia
Julai hadi Novemba 2014, sawa na pungufu kwa jumla ya dila 249 kwa tani.
Ngamlagosi alisema mafuta ya dizeli kwa lita moja yatauzwa sh.1846 na kuwa bei hiyo imeshuka kwa asilimia 13 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.244 kwa lita na kuwa dizeli kwa soko la dunia imeshuka kwa jumla ya asilimia 28 kuanzia Julai hadi Novemba 2014 sawa na pungufu kwa jumla ya dola 189 kwa tani na kuwa mafuta ya taa yatauzwa sh. sh.1833 kwa lita.
Ngamlagosi alisema mafuta ya dizeli kwa lita moja yatauzwa sh.1846 na kuwa bei hiyo imeshuka kwa asilimia 13 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.244 kwa lita na kuwa dizeli kwa soko la dunia imeshuka kwa jumla ya asilimia 28 kuanzia Julai hadi Novemba 2014 sawa na pungufu kwa jumla ya dola 189 kwa tani na kuwa mafuta ya taa yatauzwa sh. sh.1833 kwa lita.
Alisema
katika kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba
2014, bei za mafuta ghafi zimekuwa zikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi
cha hapo nyuma ambapo zimeshuka toka dola 100 kwa pipa hadi kufikia wastani wa
dola 60 kwa pipa moja ambayo ni sawa na karibu asilimia 40.
Alisema
viwango hivyo vya bei iliyopungua ni katika soko la Dar es Salaam na mikoa
mingine bei zao zimepangwa kutokana na kuwepo kwa gharama za
usafirishaji.Ngamlagosi alitoa mwito kwa wanunuaji wa mafuta hayo kuhakikisha
wanapatiwa lisiti baada ya kununua kwani itasaidia kuwabaini wafanyabiashara
wasio waaminifu ambao wataendelea kuuza kwa bei ya zamani.
"Natoa
mwito wa kuwaomba wanunuaji wa mafuta kuhakikisha wanapewa lisiti kwani
itatusaidia kuwabaini wale wanaouza kwa bei ya juu, na pia itamsaidia mnunuzi
iwapo atauziwa mafuta yaliyochini ya kiwango na ukusanyaji wa kodi ya
serikali"
alisema Ngamlagosi.
Naye
Mkurugenzi wa Petroli, Edwin Samwel alisema Ewura imejipanga vizuri
kuhakikishha hakuna ujanja ujanja utakaojitokeza wa kudai mafuta yamekwisha au
yaliyopo yatauzwa kwa bei yaliyonunuliwa.
Alisema
mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa sheria pamoja na
kufungiwa biashara yake ingawa alisema hali hiyo haitajitokeza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “EWURA YASHUSHA BEI ZA MAFUTA....KUANZIA LEO 7.1.2015”
Post a Comment