Wednesday, January 7, 2015
GESI YAANZA KUTUMIKA TANZANIA>>>>>SOMA HAPA
Do you like this story?
Shirika la maendeleo ya
Petrol nchini Tanzania limesema kuwa Mradi wa Gesi iliyogunduliwa kusini mwa
nchi hiyo ,mkoani Mtwara umefikia asilimia 94 na tayari gesi hiyo imeanza
kutumika katika baadhi ya maeneo.
Hadi sasa kuna baadhi ya
viwanda, na mashirika ambayo yameanza kutumia gesi hiyo asilia hatua inayodaiwa
kupunguza gharama za upatikanaji wa Nishati kwa baadhi ya wakazi ambao wamekuwa
wakitumia gharama kubwa ili kupata Nishati .
Gesi yaweza kuwa ni mkombozi
na rafiki kwa mwanamke kwa kumkomboa kutokana na matumizi ya mkaa na kuni kwa
muda mrefu, hasa upande wa kuni, miaka kadhaa baadaye wanawake huwa na macho
mekundu na hivyo kuhiziwa kuwa wachawi hasa kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza Nchini
Tanzania na kushuhudia mauaji ya vikongwe yasiyokwisha.
Gesi ikiuzwa kwa gharama
nafuu itamkomboa mwanamke na hatari ya kifo,kutokana na matumizi ya nishati ya
jadi ,kuni yenye madhara maishani kutokana na dhana potufu ya ushirikina kwa
mwanamke mwenye macho mekundu kudhaniwa ni mshirikiana.
Nishati ya mkaa huharibu mazingira
kutoakana na ukatwaji miti hovyo bila ya kupanda miti,lakini nishati hiyo
imepanda bei hadi kufikia tshs elfu tisini kwa gunia lla lumbesa, na kuni nazo
ni adimu mjini, lakini kijijini nafuu kiasi kama hakuna uharibifu mkubwa wa
misitu.
Suala la miradi mikubwa kama
wa gesi hutawaliwa na rushwa na hivyo kuongeza bei ya nishati hiyo na
kusababisha watu wa hali ya chini kutomudu kunufaika na nishati hiyo na
kuonekana ni nishati ya baadhi ya watu .BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “GESI YAANZA KUTUMIKA TANZANIA>>>>>SOMA HAPA”
Post a Comment