Monday, January 19, 2015
SERIKALI YA KENYA YAKUBALI KUYARUHUSU MAGARI YA ABIRIA NA WATALII KUTOKA TANZANIA.
Do you like this story?
WAZIRI wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema serikali ya Kenya imekubali
kuyaruhusu magari ya abiria na watalii kutoka Tanzania, kuingia ndani ya Uwanja
wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Awali,
Serikali ya Kenya iliyazuia magari hayo kuingia uwanjani hapo huku ukiyatoza
ushuru kwa yale yanayoingia, jambo ambalo lililalamikiwa na wafanyabiashara wa
Tanzania.
Marufuku hiyo
ya Kenya kwa magari ya Tanzania, ilidumu kwa zaidi ya wiki mbili, ambapo katika
kusaka suluhu hiyo Nyalandu alikutana na wafanyabiashara hao jijini Arusha
kisha kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya,
Phyllis Kandie.
Katika
mazungumzo yake na Kandie, Nyalandu alisema kwa sasa magari ya Tanzania
yataendelea kuingia uwanjani hapo wakati ufumbuzi wa kudumu ukitafutwa.
Alisema
kutakuwa na vikao vya kazi baaina ya Wizara ya Utalii ya Kenya na wizara yake,
ambapo vitaanzia ngazi ya watandaji, watalaamu, makatibu wakuu na
mawaziri.Alisema katika mikutano hiyo masuala mbalimbali kuhusiana na biashara
ya utalii yatazungumzwa baina ya nchi hizo mbili.
Hata hivyo,
alisema katika vikao hivyo suala la mpaka wa Bolongoja halitajaliwa wala kuwepo
kwenye ajenda.
“Kwa sasa
wafanyabiashara wetu wataingia Jomo Kenyatta kama ilivyokuwa awali.
Tumezungumza na kupanga kuwa na vikao kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto
zote kuhusiana na sekta ya utalii.“Niwahakikishie tu katika vikao hivyo maslahi
ya pande zote yatazingatiwa, lakini suala la mpaka wa Bolongoja halitajadiliwa
wala kuwemo kwenye ajenda za vikao vyetu.“Wataalamu na watendaji wa wizara
yangu watakutana na wenzao jijini Arusha na maofisa wa Jumuia ya Afrika
Mashariki watashiriki ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu,” alisema Nyalandu.
Kupatiwa
ufumbuzi kwa tatizo hilo kumekuwa faraja kubwa kwa wafanyabiashara na wadau wa
utalii katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, ambapo walipongeza jitihada za
haraka zilizofanywa na Nyalandu.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wadau
hao wa utalii walisema Nyalandu ameonyesha utendaji kazi kwa vitendo na kwamba,
hilo linapaswa kuwa mfano kwa viongozi wengine.
Walisema
waziri huyo baada ya kupata taarifa za wafanyabiashara wa Tanzania kuzuiwa
kuingiza magari Jomo Kenyatta, aliwafuata kwenye maeneo yao na kuwasikiliza kero
zinazowakabili kisha kufunga safari kukutana na waziri Kandie jijini Nairobi.
“Hawa ndio
aina ya viongozi ambao Tanzania ya sasa na inayokuja inawahitaji, wanaposikia
wananchi wana kero na wananyimwa haki ama kunyanyaswa wanakwenda kuwasikiliza
na kutafuta ufumbuzi wa haraka. “Kwa hili Waziri Nyalandu anastahili pongezi na
viongozi wengine waige mfano huu, wangekuwa wengine wangeanza kuleta siasa na
tatizo kuchukua muda mrefu kupata ufumbuzi,” alisema John Mlay, ambaye ni mmoja
wa wafanyakazi kwenye kampuni za usafirishaji watalii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YA KENYA YAKUBALI KUYARUHUSU MAGARI YA ABIRIA NA WATALII KUTOKA TANZANIA.”
Post a Comment