Monday, February 23, 2015

KAPOMBEA APIGIA ‘SALUTI’ MUZIKI WA PRISONS


MCHEZAJI kiraka wa Azam fc, Shomari Salum Kapombe amesema matokeo mabaya wanayopata Prisons ndio chanzo cha kuwakazia jana usiku katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyomalizika kwa suluhu uwanja wa Azam Complex.

“Prisons walifungwa mechi iliyopita na Yanga, leo wamekuja na nguvu. Wameonesha kiwango kizuri na nidhamu ya mchezo. Wamejilinda vizuri na kucheza mpira”.

“Tumejitahidi kufika mara nyingi golini kwao, lakini kipa wao (Mohammed Yusuph) amekuwa imara”.
Kwa matokeo ya jana, Azam fc wanaendelea kushika nafasi ya pili kwa pointi 27 baada ya kushuka dimbani mara 15, wakati Yanga wanaongoza msimamo kwa pointi 31 baada ya kucheza mechi 15.

Kapombe amesema baada ya mechi hiyo, sasa wanaelekea macho yao katika mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merreick.

Mechi ya kwanza Azam walishinda 2-0 na mechi ya marudiano itayopigwa mwishoni mwa wiki hii, matajiri wa Dar wanahitaji ushindi au kufungwa magoli yasiyozidi mawili.

0 Responses to “KAPOMBEA APIGIA ‘SALUTI’ MUZIKI WA PRISONS”

Post a Comment

More to Read