Tuesday, February 17, 2015

KOCHA SIMBA SC ATUA AFC LEOPARDS YA KENYA.




Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Ukimuona wa nini, wenzako wanasema watampata lini! Aliyekuwa kocha mkuu wa Simba SC Mcroatia Zdrvako Logarusic anatarajiwa kutua nchini Kenya wiki hii na kuanza kazi rasmi ya kuinoa timu yakje mpya ya AFC Leopards.

Ijumaa, Leopards walithibitisha kumteua Mcroatia huyo kuwa kocha mkuu wa timu yao akirithi mikoba ya Mdachi, Pieter De Jongh ambaye amefukuzwa na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Kenya.

Ingwe kupitia kwa Katibu wake Timothy Lilumbi imethibitisha kwamba Logarusic, maarufu Loga atatua nchini humo wiki hii na kuanza kazi rasmi.

"Tuko katika hatua za mwisho za kumtumia Loga tiketi ya ndege, na tunatarajia kumuona nchini ndani ya wiki hii. Ataanza kutekeleza majukumu ya timu mara tu baada ya kuwasili," amesema.

Kocha huyo wa zamani wa Gor Mahia amekaa bila timu tangu Agosti 2014 alipofukuzwa na uongozi mpya wa Simba SC, chini ya Rais Evans Aveva kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na utovu wa nidhamu.

Akiwa Tanzania, Loga alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baadhi ya wasanii wa filamu, jambo ambalo lilidaiwa kuuchafua uongozi wa Simba SC kwa vile kocha huyo alifikia hatua ya kukacha mazoezi ya timu ili ale raha na mademu hao wa Bongo Movie.

0 Responses to “KOCHA SIMBA SC ATUA AFC LEOPARDS YA KENYA.”

Post a Comment

More to Read