Cha
ajabu, sanjari na kundi hilo linalodai liko Tanga, Tanga hukohuko kwenye
Kitongoji cha Amboni, Ijumaa iliyopita kulizuka mapigano kati ya polisi, askari
wa JWTZ wakipambana na kundi lililodhaniwa ni la kigaidi likiwa limepiga makazi
ndani ya mapango ya kihistoria ya Amboni, Uwazi lina full story.
Katika mapigano hayo hadi juzi Jumapili, askari mmoja wa JWTZ aliuawa huku
wanajeshi watatu na askari polisi wawili wakijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya
Mkoa wa Tanga, Bombo.
MASHUHUDA
WA MAPIGANO
Kabla Uwazi halijatiririka na video hiyo, lilizungumza na wananchi wenye makazi
yao kwenye Kitongoji cha Amboni ambako mapigano ya askari na wahalifu
yalitokea.
Mzee Ibrahimu Ally, yeye anasema: Siku ya tukio (Ijumaa asubuhi) mimi nilikuwa
nimepumzika ndani kwangu lakini ghafla nikasikia mlio wa risasi kama mara mbili
hivi.
Mke
wangu alikuwa anafua, akaja mbio ndani akisema ni majambazi. Nilimwambia funga
mlango haraka sana, akaufunga. Lakini cha ajabu milio ya risasi ikawa
inaongezeka kadiri muda ulivyokwenda.
Ilifika mahali nikajua si majambazi bali tumevamiwa na majeshi ya nje ya nchi.
Kwani sasa risasi zilikuwa zikirindima kila muda. Hali ikawa tete kwa kweli.
Hata hapa ninapoongea na wewe siamini kama ile milio ya risasi haitajirudia
tena.
WAZIKIMBIA
NYUMBA
Mwanahawa Mudale yeye alisema: Ilibidi tuhame majumba kwenda kujificha, tatizo
ni ile milio ya mabomu na risasi na baadaye tukaona chopa (helikopta) ikitembea
angani. Awali tulijua ni vita ya nchi na nchi, kumbe walikuwa askari wetu.
SIKU
MBILI HAKUNA KULALA
Baadhi ya mashuhuda wanasema kutokana na milio ya risasi kwa siku ya Ijumaa
hadi Jumamosi asubuhi, hakuna mwananchi aliyepata usingizi.
Mimi
na familia yangu hatujalala jamani. Risasi na mabomu yasikieni hivihivi tu.
Kuna wakati tulikuwa tukiona miale ya moto kutokea kwenye eneo la mapango.
Wakati mwingine badala ya moto tuliona moshi mkubwa.
Kumbe wanajeshi wetu nao walishafika kupambana na hao watu, alisema Simeon
Patrick, mkazi wa Kitongoji cha Karasha, Amboni.
INAVYODAIWA
Habari zilizosambaa juzi, zinadaiwa kundi hilo lililopambana na askari ni la
kigaidi ambapo safari yao kubwa ilikuwa kwenda kufanya ugaidi wa kumwaga damu
nchi jirani ya Kenya.
Wale
jamaa nasikia walikuwa wakipeleka vifaa nchini Kenya eneo la mwambao ili waje
wafanye uhalifu baadaye.
Sasa wakiwa katika hatua za mwisho mwisho baada ya kupeleka silaha za kivita,
wakashtukiwa. Ikabidi waache silala zao eneo walipozificha na wao waje Tanga
kujificha kwenye mapango.
Lengo
lao, watulie mpaka hali kule Kenya itakapokuwa imepoa ndipo wajitokeze. Sasa
kilichotokea ni kwamba, wakati wanaishi mapangoni ilibidi waanze kutoka
kutafuta chakula kwa kufanya uhalifu mdogomdogo ndipo siku moja jamaa yao mmoja
akakamatwa kwa uhalifu.
Yule
jamaa ndiye aliyewapeleka polisi walipo wenzake na kutokea kwa mapigano makali
kama yale, alisema mtoa habari mmoja huku akiomba jina lake lihifadhiwe.
KUHUSU
VIDEO MPYA
Tukiachana na mapigano ya Amboni, sasa turudi kwenye video mpya ya watu
waliojiita ni watetezi wa haki dhidi ya udhalimu.
Video hii ipo ndani ya mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wanaonekana watu
wawili wakiwa wamevaa mavazi ya kininja ili wasijulikane.
Watu
hao wanasema wanapinga jamii yao kukamatwa na kuuawa mara kwa mara wakidai
jeshi linawaonea hivyo kutangaza kupambana na askari.
Video hiyo haipishani sana na ile iliyotangulia kuandikwa kwenye gazeti ndugu
na hili la Ijumaa.
KAULI
YA JESHI LA POLISI
Akizungumza na Uwazi jijini Tanga muda mfupi baada ya kutulia kwa mapambano ya
Amboni, Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja aliwataka
wananchi kutulia na kuendelea na shughuli zao za kawaida huku akisisitiza:
Askari walifika mapangoni, kundi lile ni la majambazi. Lilianza kufanya
mashambulizi ya risasi na katika majibizano, askari sita walijeruhiwa na
kuwahishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo, amesema Kamishna
Chagonja.
0 Responses to “ TAZAMA VIDEO NYINGINE YA MAPIGANO NA MAGAIDI TANGA HII NDIYO FULL STORY”
Post a Comment