Wednesday, February 18, 2015
MAMA WA MTOTO ALBINO ALIYETEKWA GEITA AZUNGUMZA ALIVYOJERUHIWA NA KUPORWA MTOTO.
Do you like this story?
MAMA wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi,
Yojana Bahati (1), Ester Thomas aliyelazwa katika hospitali ya Bugando
akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa, ameelezea jinsi alivyovamiwa na watu
wasiojulikana.
Akizungumza na mwandishi wetu, Ester
(30) alisema alijeruhiwa juzi nyakati za usiku na watu wasiojulikana mkoani
Geita baada ya kumvamia nyumbani kwao na kumpora mtoto wake mwenye ulemavu wa
ngozi.
Akizungumza kwa shida hospitalini hapo,
Ester alisema alivamiwa akiwa amelala na mtoto wake huyo ambapo walimkatakata
kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na kisha kutokomea kusikojulikana.
Naye Mkuu wa kitengo cha dharura
hospitalini hapo, Dk Derick David alisema mgonjwa huyo alipokewa juzi saa nane
mchana akitokea mkoani Geita.
Daktari alisema mgonjwa huyo ambaye
hali yake sio ya kuridhisha, alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana na
kukatwa panga kwenye paji la uso pamoja na kukata sehemu ya mfupa wa pua.
“Tunamshukuru Mungu mgonjwa huyu
anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji kwani kwa sasa hali yake ni
tofauti na alivyopokewa,” alisema.
Alisema mama huyo anaendelea na
matibabu ya majeraha na pia atapatiwa na huduma ya kisaikolojia kutokana na
maumivu makali aliyonayo ya kuporwa kwa mtoto wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAMA WA MTOTO ALBINO ALIYETEKWA GEITA AZUNGUMZA ALIVYOJERUHIWA NA KUPORWA MTOTO.”
Post a Comment