Wednesday, February 18, 2015

MVUA YAHARIBU HEKTA 62 ZA MAHARAGE MBOZI.




Na Saimeni Mgalula,Mbeya
Jumla ya hekta 62  za Maharage pamoja na 148 mahindi na 168 za kahawa zimeharibiwa vibaya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji cha Isansa Wilaya Mbozi Mkoani Mbeya.

Mvua hiyo ilinyesha takribani dakika 45 ambayo ilianza kunyesha kuanzia saa 9:00 mpaka 9:45 arasili  ambapo ’iliambatana na mawe makubwa na kusababisha uhalibifu huo .

Kutokana na hali hiyo Wakazi wa kijiji hicho  wameiomba serikali kuwapatia msaada wa chakaula cha mahindi kutokana na Mazao yao kuharibiwa na mvua hiyo .

Akizungumzia maafa hayo ,Afisa kilimo wa Wilaya ya Mbozi Richard Silinde amesema inawezekana kukawa na njaa kutokana na mvua hiyo kuharibu mazao kwa kiasi kikubwa sana katika kijiji hicho.

Amesema  mazao ambayo yameharibiwa na mvua hiyo ni Kahawa ,Mahindi ambayo yalikuwa yanaanza kubeba watoto na Zao la Maharage ambalo ndio limeharibiwa vibaya.

Amesema kuwa pia kuna baadhi ya Kaya ziliaribiwa na mvua hiyo kwa kutobolewa mabati ambayo yameezekwa  ambapo pia hakukuwa na madhara yeyote kwa binadam.

Afisa huyo amesema kutokana na maafa hayo Serikali inafanya taratibu kwa kina juu ya tatizo hilo na mara baada ya kumaliza taratibu hizo tutawakilisha taarifa nzima katika kamati ya Pembe Jeo ili baadhi ya wakulima wapewe mbegu  kutokana na kuwepo kwa mbegu fupi.


0 Responses to “MVUA YAHARIBU HEKTA 62 ZA MAHARAGE MBOZI.”

Post a Comment

More to Read