Tuesday, February 24, 2015
MBUNGE AZUA BALAA NA NGUO YA NDANI INAYOMBANA NDANI YA KIKAO CHA BUNGE.
Do you like this story?
Kumekuwa na matukio mengi yanayotokea
ndani ya Mabunge mbalimbali duniani halafu yanachukua headlines kubwa mtaani na
mitandaoni, tumeona ya TZ, Kenya, Afrika Kusini ile juzi wakati Rais Zuma akiwa
anahutubia, hii nakupa na wewe uipate kutoka ndani ya Mjengo wa Bunge Canada.
Mbunge Pat
Martin naye katoa kali ya mwaka, ile story yake aliyoitoa yani
hakuna Mbunge ambaye hakucheka.
Kulikuwa na ishu ya kupiga kura
ikiendelea ndani ya Bunge hilo, Mbunge huyo akahojiwa sababu iliyomfanya awe
nje ya Jengo wakati zoezi la kura likiendelea, katika kujitetea akajibu kwamba
alijikuta akilazimika kutoka nje ya kikao kutokana na nguo ya ndani aliyokuwa
ameivaa ilikuwa ikimbana sana hivyo asingeweza kuvumilia kuendelea kukaa ndani
ya kikao hicho.
Pat Martin alijitetea
kwamba anadhani kilichomponza ni kitu ambacho kimewaponza wengi pia ishu ya
kutaka kununua vitu vya bei poa ama kuomba kupunguziwa bei za vitu.
Yeye alinunua nguo hizo za ndani nyingi
baada ya kuzikuta zikiuzwa kwa nusu bei, akanunua nyingi bila hata kujua kama
zilikuwa zinamtosha size au hapana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBUNGE AZUA BALAA NA NGUO YA NDANI INAYOMBANA NDANI YA KIKAO CHA BUNGE.”
Post a Comment