Tuesday, February 24, 2015
SAFARI LAGER YATANGAZA BAR 5 ZILIZOINGIA FAINALI NYAMA CHOMA MBEYA 2015.
Do you like this story?
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoli |
Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoliakizungumza na vyombo vya habari alipokuwa akitangaza Bar zilizotinga fainali ya Safari lager nyama choma. |
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya
Safari Lager imetangaza bar tano
zilizofanikiwa kuingia fainali kwenye kinyang’anyiro cha shindano lauchomaji
nyama Mkoani Mbeya lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition
2015”.
Akizungumza na waandishi wa
habari, katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mikuyu, Meneja
matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoli alisema Bar
zilizofanikiwa kutinga fainali zimepatikana kutokana na kura zilizopigwa na
wateja wao.
Masoli alizitaja bar zilizoifanikiwa kuingia fainali
kuwa ni pamoja na Karembo Bar iliyoko Sokomatola,New City Pub iliyopo
Mwanjelwa,Tumaini Bar iliyopo Ilomba,Samaki Samaki Bar iliyopo Forest ya zamani
na Nebana Bar iliyopo Soweto jijini Mbeya.
Alisema fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma
mwaka huu wa 2015 zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Chuo cha Uhasibu
(TIA) jijini Mbeya Februari 28,kuanzia saa mbili asubuhi na kuendelea
zikisindikizwa na Bendi ya TOT, na
burudani zingine nyingi pamoja na zawadi kemkem kutoka Safari Lager.
Alisema shindano hili
hufanyika kila mwaka,ambapo kwa mwaka
huu linafanyika kwa mara ya nane mfululizo
huku yakizinduliwa katika Mkoa wa Mbeya na kufuatiwa na mikoa ya Mwanza,
Arusha, Kilimanjaro na mwisho Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa tangu
lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hilo limekuwa na mvuto wa kipekee kwa
wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa
wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa
waliopo.
“Lengo kuu la shindano la
Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa
nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora vya uchomaji na
utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa
yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa
mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma”alisema Masoli na kuongeza.
“Tumezingatia maombi ya
washiriki wa mwaka jana hivyo basi mwaka
huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji nyama itafanyika kwa bar zote
zinazoshiriki na wala sio baa chache zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka
ya nyuma”.
Alisema washiriki watapimwa ujuzi wao katika
kutayarisha nyama choma za aina tatu ambazo ni
nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.
Alizitaja zawadi watakazopata washindi walioingia katika fainali na
kuibuka na ushindi kuwa ni Mshindi wa kwanza ambaye ni Bingwa wa
Mkoa atapata shilingi 1,000 000/=, Mshindi
wa pili shilingi 800,000/=,Mshindi wa tatu shilingi 600,000/=, mshindi
wa nne 400,000/= na mshindi wa tano
200,000/=.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SAFARI LAGER YATANGAZA BAR 5 ZILIZOINGIA FAINALI NYAMA CHOMA MBEYA 2015. ”
Post a Comment