Saturday, February 21, 2015

MVUA YALETA MAAFA MBEYA.
















Afisa Elimu Shule za Msingi Jiji Bi Auleria Lwensa akiongea na wanafunzi



Waalimu wa Shule hiyo wakitoa mabati ambayo yaliyoezuliwa na Mvua

                                      (Picha na Fahari News)


Mvua za masika zinazoendelea kunyesha nchini Tanzania leo hii zimezua balaa baada ya mvua kubwa iliyoambatana upepo mkali kunyesha katika maeneo mbalimbali jijini Mbeya na kuleta maafa. Kati ya maeneo yaliyoathiriwa na mvua hiyo ni pamoja na Ilemi jijini Mbeya ambapo takribani kaya 40 pamoja na shule zimeezuliwa, huku wanafunzi wawili wa shule ya msingi Ilemi wakijeruhiwa kwa kuangukiwa na kuta za shule hiyo.

Mashuhuda wa mvua hiyo iliyonyesha kwa karibu dakika 20 mchana majira ya saa nane wameeleza kuwa mvua hiyo iliambatana na upepo mkali ambao uliweza kuangusha kuta pamoja na miti na kuhatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo. Kuhusiana na shule zilizoathiriwa na balaa hilo, Vyumba vya madarasa, ofisi na vyoo vimeezuliwa na upepo na baadhi ya kuta kudondoka ambapo Afisa Elimu jiji la Mbeya kwa shule za msingi, Auleria Lwensa msingi ambaye alifika katika eneo la tukio amewataka waalimu na wanafunzi kuendelea kuyatumia madarasa na ofisi ambayo hayajaathiriwa.

 Pamoja na hayo bi. Auleria amesema kuwa shule haitafungwa na badala yake masomo yataendelea huku ukifanywa utaratibu na bodi ya shule ili kuwezesha ukarabati wa majengo hayo huku akiwataka wakazi wa maeneo hayo kupeana msaada unaowezekana kwa zile familia zilizoathirika na janga hilo kwakuwa ni jambo la dharura.





0 Responses to “MVUA YALETA MAAFA MBEYA.”

Post a Comment

More to Read