Tuesday, March 3, 2015
KIGOGO MWANZA MBARONI KWA MAUAJI YA ALBINO.
Do you like this story?
KIONGOZI wa chama
kimoja cha siasa mkoani Mwanza (jina tunalo) anashikiliwa na Jeshi la Polisi
akihusishwa na uhalifu wa utengenezaji wa noti bandia, utekaji na mauaji ya
albino katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa.
Habari za uhakika
zilizolifikia MTANZANIA kutoka vyanzo vyetu vya habari zimesema kuwa kigogo
huyo alikamatwa wilayani Magu Februari 26, mwaka huu saa 7:00 usiku.
Kigogo huyo
ambaye anadaiwa kuhusishwa na utekaji wa mauaji ya albino alikamatwa baada ya
kutajwa na washirika wake katika matukio waliyofanya katika sehemu mbalimbali
za mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Habari zaidi
zilieleza kuwa kigogo huyo anahusishwa kwa karibu na matukio ya hivi karibuni
yaliyotokea katika mikoa ya Mwanza na Geita ambako watoto wawili Pendo Emmanuel
(4) mkazi wa Ndami Kwimba (Mwanza)na Yohana Bahati (1) wa Ilyamchele, Chato
mkoani Geita.
“Mtuhumiwa
alikamatwa na makachero wa polisi nyumbani kwake kabla ya kusafirishwa hadi
Mwanza anakoshikiliwa hadi sasa na wakati anapekuliwa nyumbani kwake alikutwa
na noti bandia,” kilieleza chanzo chetu.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alipoulizwa alisema kwa sasa yuko nje ya
ofisi, hawezi kuthibitisha na kuahidi hadi atakapokuwa ofisini leo.
“Taarifa hiyo
unayoniuliza kwa sasa sina, sina taarifa hiyo na siwezi kuizungumzia, kwa sasa
niko nje ya ofisi naomba tuwasiliane (kesho) leo,”alisema Mlowola.
Februari 14 mwaka
huu wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo
alisema watuhumiwa 15 wanaodaiwa kuhusika kumteka na kumsafirisha Pendo
Emmanuel hadi hoteli moja jijini hapa walikuwa wakishikiliwa na Polisi.
Chanzo:Mtanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIGOGO MWANZA MBARONI KWA MAUAJI YA ALBINO.”
Post a Comment