Wednesday, March 4, 2015
MWALIMU ALIYEKUWA AKIISHI NA KINYESI NDANI KWA MIAKA MIWILI, AKIMBIZWA MUHIMBILI.
Do you like this story?
Mwalimu wa shule ya Sekondari Kibasila,
Gaudensia Albert aliyekuwa akihifadhi kinyesi ndani kwake kwa miaka miwili
amepelekwa Hospitali ya Muhimbili baada ya daktari wa Hospitali ya Temeke
kubaini ana matatizo ya akili.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo,
Kyando amesema baada ya kugundulika kwa tukio hilo walimpeleka Hospitali ya
Temeke kwa kuangalia afya yake ambapo daktari akasema ana tatizo la akili,
wakamuhamishia Muhimbili.
Baada ya kufikishwa Muhimbili madaktari
walimpatia dawa ambazo anatumia mpaka sasa pamoja na ushauri.
“Sisi bado tunamhitaji kutokana na
tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi ulioko nchini”—alisema Mwalimu
Kyando
na kuongeza kuwa mbali na tatizo la kukutwa na kinyesi bado mwalimu huyo
alikuwa anafundisha vizuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWALIMU ALIYEKUWA AKIISHI NA KINYESI NDANI KWA MIAKA MIWILI, AKIMBIZWA MUHIMBILI.”
Post a Comment