Tuesday, March 3, 2015
WATU 3 WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI WILAYA YA CHATO KUSOMEWA SHITAKA LA MAUAJI YA MTOTO ALBINO YOHANA BAHATI.
Do you like this story?
Watu watatu wamefikishwa mahakama ya
wilaya ya Chato kusomewa shitaka la mauaji ya mtoto Yohana Bahati aliyeibiwa
hatimaye kuuwawa tarehe 15 Februali katika kitongoji cha mapinduzi wilayani
Chato mkoani Geita.
Akizungumza
na waandishi wa habari, kamanda wa polisi mkoa wa Geita Sacp Joseph konyo
amesema watu wengine wawili bado wanahojiwa na jeshi la polisi ili kupata
ushahidi unaojitosheleza katika kesi hiyo, amewataja watu waliofikishwa
mahakamani ni Bahati Misalaba ambaye ni baba wa Yohana, Juma Lupembe Kilebelo,
Manyanda Mandege almaarufu Makongoro mkazi wa wilaya ya Mbogwe na mchimbaji wa
dhahabu.
Kamanda
konyo amesema jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kuwakamata wauwaji wa
kukodiwa wanaofanya mauaji hayo kwa ujira mdogo wa laki moja ili kudhibiti
vitendo vya mauaji katika maeneo ya kanda ya ziwa.
Katika
tukio jingine jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani
watu watatu wanaosadikika kuwa ni majambazi wazoefu wa kuteka magari barabarani
na kuvamia maduka ya fedha mkoani Geita, watu hao Niosca John Bosco, Kapuru
Msigwa ustaadhi, na Elias Shigilimelo Bambala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATU 3 WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI WILAYA YA CHATO KUSOMEWA SHITAKA LA MAUAJI YA MTOTO ALBINO YOHANA BAHATI.”
Post a Comment