Thursday, June 25, 2015
AFRIKA KUSINI HUENDA IKAJIONDOA KWENYE ICC.
Do you like this story?
Afrika
Kusini imesema kuwa huenda ikajiondoa kutoka kwa mahakama ya kimataifa ya
uhalifu wa kivita ICC yenye makao yake makuu huko Hague Uholanzi kufuatia
jaribio la kumkamata rais wa Sudan Omar al Bashir alipokuwa nchini humo majuzi.
Hata
hivyo Nusra akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa
kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Lakini
baada ya kikao maalum cha baraza la mawaziri nchini humo, serikali ilitoa onyo
kuwa huenda ikalazimika kujiondoa kutoka kwa makubaliano yeyote na mahakama ya
ICC kutokana na sababu kadha.
Rais huyo wa
Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa bara Afrika
''Serikali
inawajibu wake wa kimataifa lakini pia inawajibu wake kisiasa''taarifa hiyo
ilisema.
''iwapo
hatutakuwa na suluhisho maalum itakayotusaidia kutanzua taharuki iliyopo kwa
sasa nafikiri serikali yetu haitakuwa na budi ila kujiondoa kutokana na
makubaliano yeyote na ICC''iliendelea kusema.
Mahakama
ya Afrika Kusini ilikuwa imemuagiza rais Bashir kusalia nchini humo huku
ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo la kukamatwa kwake litekelezwe au la.
Lakini
kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake rais Bashir aliondoka nchini Afrika
Kusini na kurejea nyumbani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ AFRIKA KUSINI HUENDA IKAJIONDOA KWENYE ICC.”
Post a Comment