Thursday, June 25, 2015

SUALA LA MAHAKAMA KUMPA MBUNGE SUGU MWANAYE AMLEE LAIBUKA BUNGENI DODOMA.


Mh Martha Mlata akiongelea suala hilo bungeni.


Mbunge wa viti maalum Mh Martha Mlata (CCM) ameliingiza suala la Mahakama ya Mwanzo Manzese Sinza kuamuru Mbunge wa Mbeya mjiji Mh Joseph Mbilinyi "Sugu" apewe mtoto wake kutoka kwa mama yake.

Suala hilo limeibuka bungeni na mbunge huyo kudai kuwa Mh Sugu amemnyanyasa mwanamke hivyo kumtaka mbunge huyo amrudishe mtoto kwa mama yake.

"Napenda kuwaomba wateteaji wa haki za binadamu na haki za watoto kuingilia kati suala hili, Mbunge huyu aliyemnyang'anya Feiza mtoto wa miaka miwili amrudishie maana si haki hata kidogo" amesema mbunge huyo

Hali hiyo ilionekana kumchefua Mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila na kumtaka mbunge huyo kuheshimu uamuzi wa mahakama, huku Spika Anna makinda akimkataza kuzungumzia suala hilo na kumtaka ajikite kwenye mada inayojadiliwa 

Hivi karibuni Mbunge huyo alimburuza mahakamani mzazi mwenzie kwa madai kuwa ameshindwa kumlea mtoto wao kwa madai ya kupiga picha za utupu zitakazomfundisha maadili mabaya

0 Responses to “ SUALA LA MAHAKAMA KUMPA MBUNGE SUGU MWANAYE AMLEE LAIBUKA BUNGENI DODOMA.”

Post a Comment

More to Read