Tuesday, June 23, 2015
RWANDA YASHTUMU KUKAMATWA KWA AFISA WAKE.
Do you like this story?
Rwanda imeshutumu
uamuzi wa mamlaka za Uingereza kumkamata kiongozi wake wa ujasusi wa Rwanda,
Karenzi Karake, ambaye anatakiwa Uhispania kwa madai ya uhalifu wa kivita.
Waziri wa maswala ya kigeni Louis Mushikwabo
ameelezea hatua hiyo kama wazimu na lengo lake ni kukandamiza waafrika
akiongezea kwamba inatokana na madai ya watu wanaotaka kuwanyima haki waathiriwa
wa mauaji ya kimbari nchini humo mwaka 1994.
Mamlaka ya Uhispania inataka kumhoji bwana
Karake kuhusu kuhusika kwake katika mauaji ya raia wakiwemo wafanyikazi wa
msaada kutoka Uhispania baada ya mauaji hayo.
Kesi ya Uhispania ilianzishwa mwaka 2008,lakini
waandishi wanasema kuna wasiwasi kuhusu ushahidi wa mashtaka.
Makumi ya maelfu ya raia wa Rwanda wanadaiwa
kufariki baada ya mauaji hayo ya kimbari aidha kupitia mauaji ya kulipiza
kisasi nchini Rwanda ama katika kile waandishi wanataja kama wimbi la mauaji ya
kikabila katika taifa jirani la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya
wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda kuwalazimisha raia wa kabila
la Hutu kutoka katika kambi za wakimbizi karibu na mpaka.
Takriban watu laki nane hususan wale wa
kabila la Tutsi waliuawa na wenzao wa kabila la Hutu katika mauaji ya kimbari
yaliochukua miezi mitatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ RWANDA YASHTUMU KUKAMATWA KWA AFISA WAKE.”
Post a Comment