Monday, September 21, 2015
DR.JOHN POMBE MAGUFULI: SITAKUA DIKTETA NITAFUATA UTAWALA WA SHERIA NITAKAPOKUWA MADARAKANI
Do you like this story?
![]() |
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano huo mjini Chato. |
![]() |
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wana Chato na kumuombea kura mumewe pamoja na wabunge wa CCMna Madiwani. |
![]() |
Ali Tumbo akapanda jukwaani na Mbuzi akisakata muziki ili mradi burudani tu. |
![]() |
Kundi la Orijino Kemodi wakionyesha vichekesho vyao jukwaani. |
![]() |
Yamoto Band wakifanya vitu vyao jukwani. |
Mji wa Chato na viunga
vyake umetikisika huku shughuli zikisimama wakati mgombea urais wa chama cha
mapinduzi Dr.John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi wa mji huo
na miji ya jirani.
Mgombea huyu wa kiti
cha urais kupitia chama cha mapinduzi CCM ambaye pia amekuwa mbunge wa jimbo la
Chato kwa miaka 20 na kulinawirisha kwa maendeleo kadhaa licha ya changamoto
zilizopo amepata mapokezi yasiyo na kifani mjini Chato ambapo akizungumza na
mamia kwa maelfu ya wakazi hao waliojaa katika viwanja vya shule ya sekondari
Chato amewaambia watanzania endapo atapewa ridhaa ya kuwa rais wa jamhuri ya
muungano amepania kuifanya Tanzania kuwa na uchumi unaotegemea viwanda na kwa
kuanzia viwanda vyote vilivyobinafsishwa na kushindwa kuendelezwa na wahusika
atavirejesha mikononi mwa serikali na kuvifufua.
Dr Magufuli pia
amewataahadharisha wakazi wa Chato na mikoa ya kanda ya ziwa inayozungukwa na
ziwa Victoria kuvua kistaarabu bila ya kutumia sumu aina ya Thiodan ili samaki
waendelee kuzaliana kwa wingi na kuwanufaisha kiuchumi wakazi wanaozungukwa na
ziwa Victoria na kuwaahidi kuwasaidia kwa kuwapatia ruzuku na mahitaji mengine
yatakayosaidia uvuvi.
Aidha Dr Magufuli
amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii na maarifa kwa kuwa hata katika
biblia imeandkwa asiyefanya kazi na asile na kwamba jukumu lake litakuwa ni
kusimamia kikamilifu na kwa uaminifu rasilimali na maliasili za nchi kwa faida
ya watanzania wote na kwamba ataendesha nchi kwa kuzingatia misingi ya sheria
na utawala bora.
Awali akizungumza na
wakazi wa Chato kabla ya kumwalika Dr Magufuli kuzungumza na hadhira
iliyokusanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Chato kiongozi wa
msafara wa kampeni alhaji Abdalah Bulembo amesema CCM iko tayari kwa midahalo
itakayowashirikisha wagombea urais kama umoja wa katiba ya wananchi UKAWA
wanavyotaka na kwamba Dr Magufuli yuko tayari wakati wowote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DR.JOHN POMBE MAGUFULI: SITAKUA DIKTETA NITAFUATA UTAWALA WA SHERIA NITAKAPOKUWA MADARAKANI”
Post a Comment