Monday, September 21, 2015
MABASI 138 YA BRT YATUA DAR.
Do you like this story?
Mabasi
138 ya Mwendo Kasi (BRT), yamewasili katika Bandari ya Dar es Salaam kutoka
nchini China. Kuwasili kwa mabasi hayo kutasaidia kupunguza tatizo la usafiri
katika Jiji la Dar es Salaam.
Katika
Bandari ya Dar es Salaam kutoka China tayari kwa huduma ya usafiri. Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, aliwaambia waandishi wa habari
jana baada ya kufanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili
kwa mabasi hayo.
“Tumefikia
hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya Uda Rapid Transit (Uda-RT) kwa kuleta
mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri katika kipindi cha
mpito. Hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili,” alisema.
Alisema
serikali ilifanya kazi kubwa kuunganisha Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na
wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya Uda-RT.
Hata
hivyo, alisema taarifa za nauli za mabasi hayo ya Sh. 900 zilizotolewa
katika mtandano, zilikuwa ni uzushi na upotoshaji.
Alisema
suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya
Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na hivyo uzushi huo umewaletea
usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa kuwapuuzia.
Msemaji wa
Kampuni ya Uda-RT, Subri Maburuki, alisema mabasi yote yameingia yakiwamo ya
mita 12 yapo 101 na mita 18 yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha mpito
kitaanza baada ya kukamilisha taratibu za bandari.
“Tuliahidi
kuwa mwezi huu mabasi yatakuwa yamewasili na ni kweli yamekuja, kwa pamoja na
yale ya kufundishi yatakuwa mabasi 140,” alifafanua Maburuki.
Kaimu
Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga, alisema meli iliyobeba mabasi
hayo ilipitia Kenya na kimsingi kutokea nchini China, ilikuwa imebeba magari
1,700 yakiwamo mabasi ya Uda-RT.
CHANZO:
NIPASHE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MABASI 138 YA BRT YATUA DAR.”
Post a Comment