Monday, September 21, 2015
RAIS KENYATTA: HATUWEZI KULIPA WALIMU
Do you like this story?
![]() |
| Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. |
![]() |
| Mgomo wa walimu nchini Kenya |
Wakati
shule zote za serikali na za binafsi nchini Kenya zikianza kufungwa kuanzia hii
leo, rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta akihutubia taifa hilo kwa njia ya
televisheni amesisitiza kuwa serikali yake haina uwezo wa kulipa nyongeza ya
mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo.
Ametoa wito kuwa, mgogoro huo utatuliwe kwa
amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia leo. Serikali ya Kenya
imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu nchi
nzima ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza
shule zote za serikali na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi majumbani
mwao. Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya
kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)



0 Responses to “RAIS KENYATTA: HATUWEZI KULIPA WALIMU”
Post a Comment