Tuesday, September 29, 2015
YALIOJIRI WAKATI WA KUUAGA MWILI WA CELINA KOMBANI YAPATE HAPA.
Do you like this story?
Celina Kombani enzi za uhai wake.
|
Makamu wa Rais, Dk. Bilal akielekea
kutoa heshima za mwisho kwa Kombani
|
Anne Makinda akitoa heshima za
mwisho kuaga mwili wa Celina Kombani
|
Mama Maria Nyerere akiwa mbele ya
jeneza.
|
Huyu ni Waziri wa Habari Vijana
Utamaduni na Michezo, Fenala Mkangala
|
Msanii wa filamu Wema Sepetu akiuaga
mwili wa Kombani
|
Makamu wa rais Dk Mohamed Gharib Bilal amewaongoza
waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa waziri wa nchi, ofisi ya rais,
menejimenti ya utumishi wa umma Mh Celina Kombani zoezi lililofanyika viwanja
vya Kareemje jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Morogoro
kwa maziko.
Mara baada ya mwili huo kuwasili katika viwanja hivyo
mchungaji Wilfred Mmari ameongoza ibada fupi ya kumuombea marehemu kabla ya
makundi mbalimbali kutoa salaam zao za rambirambi.
Akisoma salamu za serikali waziri wa nchi ofisi ya waziri
mkuu sera, uratibu na bunge Mh Jenista Mhagama mbali na kueleza uadilifu
uliotukuka wa marehemu Kombani amesema ndani ya serikali ameacha pengo huku
mwakilishi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar naye akitoa salaam.
Naye spika wa bunge anayemaliza muda wake Mh Anne Makinda
akitoa salaam kwa niaba ya ofisi ya bunge amewataka watumishi wa umma kutumia
msiba huo kutafakari na kurekebisha maisha yao kwa kuwa na upendo na
kuwatumikia wananchi kwa kutoa huduma bora.
Baadhi ya mawaziri wenzake na wabunge waliojitokeza kuuaga
mwili huo wamemwelezea marehemu Kombani namna alivyokuwa mwalimu wao kila mara
walipotaka ushauri wake ndani na nje ya bunge.
Mbali na makamu wa rais baadhi ya viongozi wengine waliohudhuria
zoezi hilo ni pamoja na mawaziri, wabunge, viongozi wa vyama vya siasa, mama
Maria Nyerere na mama Salma Kikwete.
Akisoma wasifu wa marehemu mwakilishi wa serikali amesema
marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya kongosho iliyokuwa
imeathiri ini lake na alizaliwa june 19 1959 na kufarifariki dunia septemba 24
mwaka huu katika hospitali ya Apollo nchini India na mwili wake unatarajiwa
kuzikwa sept 29 mkoani Morogoro na ameacha mume,watoto watano na wajukuu wanne.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ YALIOJIRI WAKATI WA KUUAGA MWILI WA CELINA KOMBANI YAPATE HAPA.”
Post a Comment