Tuesday, September 29, 2015

-RAIS KIKWETE ATANGAZA HATUA 5 MUHIMU ZITAKAZOCHUKULIWA JUU YA HAKI ZA WANAWAKE.




Tanzania imeahidi kuchukua hatua tano muhimu za kutetetea na kuendeleza haki za wanawake kati ya sasa na mwaka 2030, ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko makubwa ya kufuta sheria zinazokandamiza wanawake na kutunga sheria za kuleta usawa wa kijinsia,ikiwa ni utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) mapya kwa manufaa ya wanawake wa Tanzania.

Miongoni mwa hatua hizo itakuwa ni pamoja na kufuta ama kufanya mabadiliko ambayo yanaendeleza vitendo vya kiutamaduni ambavyo kwavyo vinaendeleza ubaguzi wa wanawake kama vile Sheria ya Ndoa, Sheria ya Urithi na kutunga Sheria ya Kukomesha Ukatili dhidi ya wanawake.

Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa mwishoni mwa na Rais Jakaya Kikwete wakati alipozungumza katika Mkutano wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Akinamama: Dhamira ya Kuchukua Hatua uliohudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali duniani kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, Marekani.

RaisKikwete ameuambia mkutano huo ulioitishwa kwa pamoja na Jamhuri ya Watu wa China, Denmark, Mexico na Kenya kuwa hatua ya pili ambayo Tanzania inakusudia kuchukua ni kuridhia makubaliano yote ya kimataifa kuhusu haki za akinamama hasa Makubaliano ya Kimataifa Juu ya Kukomesha Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake.

Hatua nyingine ambazo Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania itachukua katika miaka 15 ijayo ili kuhakikisha usawa wa kijinsia nchini hatua kadhaa ikiwemo,kuendeleza na kuunga mkono upatikanaji wa rasilimali fedha zinazolenga kuongeza usawa wa kijinsia.

0 Responses to “-RAIS KIKWETE ATANGAZA HATUA 5 MUHIMU ZITAKAZOCHUKULIWA JUU YA HAKI ZA WANAWAKE.”

Post a Comment

More to Read