Saturday, October 31, 2015
ALIYETONGOZA KUPITIA FACEBOOK AFUNGWA JELA
Do you like this story?
![]() |
Labrie Owen alikuwa akishindana na wenzake nani atashiriki ngono zaidi |
![]() |
Labrie Owen sasa sharti asajiliwe kama mtu aliyewahi kuwadhulumu watoto kijinsia |
Mwanaume mmoja 20,aliyetumia Facebook kumtongoza mwanafunzi mwenza kwa
nia ya kushiriki ngono naye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela nchini
Marekani.
Owen Labrie alipatikana na hatia ya kumtongoza msichana huyo ambaye
jina lake limebanwa kwa sababu ya umri wake mdogo wa miaka 15.
Labrie na msichana huyo walikuwa wanafunzi wa shule moja ya kifahari
sana mjini Concord, New Hampshire.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo, wakili wa mshtakiwa alidai kuwa ni
desturi ya wanafunzi wanaokamilisha masomo kuwaalika wanafunzi wapya shuleni
humo kisha wakashiriki ngono nao katika tamaduni inayojulikana kwa jina la
uzushi ''kupiga saluti''
Shule hiyo ya kifahari na ghali ya St Paul inajivunia kuwa kitovu cha
elmu kwa mamia ya viongozi wa kada mbalimbali nchini Marekani akiwemo waziri wa
maswala ya kigeni John Kerry.
Wanafunzi wengine waliosomea katika shule hiyo ya ''Kupiga saluti'' ni
mabalozi 13 na watafiti wenye hadhi ya juu duniani.
Wakili wa msischana huyo aliiambia mahakama kuwa Labrie alijigamba kwa
maswahiba wake kuwa alikuwa 'amepigia saluti' msichana huyo na hivyo
kumsababishia fedheha miongoni mwa wanafunzi wake.
Katika kujitetea wakili wa Labrie aliomba mahakama imhurumie mteja wake
kwani huo ulikuwa ujinga wa matineja waliokuwa mbioni wakitaka kukubalika na
wenzao.
Jaji wa mahakama ya juu Larry Smukler alimtaja Labrie kuwa 'muongo wa
kupindukia' alipotoa hukumu hiyo ya mwaka mmoja gerezani.
chanzo BBC Swahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ALIYETONGOZA KUPITIA FACEBOOK AFUNGWA JELA”
Post a Comment