Saturday, October 10, 2015

KIJANA MMOJA AFARIKI BAADA YA KUANGUKUWA NA JIWE




Kijana mmoja anayejulikana kwa jina la  Johnson Muchunguzi amefariki dunia baada ya kuangukiwa na miamba ya mawe alipokuwa katika shughuli za uchimbaji wa mchanga kwenye eneo la machimbo  yasiyo rasmi ya Rwome yaliyopo katika kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba,.

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kijana huyo pamoja na wenzake walikutwa na dhaama hiyo majira ya asubuhi baada ya jiwe kubwa kuanguka na kumfukia wakati akiwa katika shimo alilokuwa akichimbia mchanga.

Vikosi vya usalama pamoja na kuwahi katika  eneo la tukio havikuweza kuokoa maisha ya kijana huyo ,ambaye tayari alikuwa keshapoteza maisha kutokana na kuzidiwa na uzito wa jiwe moja lililomgandamiza kabla ya kufuatiwa na jiwe jingine lililokatisha tamaa juhudi za kumuokoa zilizokuwa zikifanywa na vikosi vya usalama pamoja na wananchi.

Baadhi ya Wananchi walioshuhudia pamoja na majirani wanaelezea kwa huzuni tukio hilo na kudai kuwa kijana huyo alikandamizwa na jiwe kubwa ambalo lilikuwa lizito kwan walipofika eneo la tukio walimkuta bado ni mzma akiomba msaada na kusema tukio hilo limewahuzunisha sana.

Katika hali ya kushangaza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Rwome Ponsian Wamala anakiri kuwepo kwa machimbo hayo  yasiyo rasmi,huku akishindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya wachimbaji hao.

Hadi chanzo cha habari hii kinaondoka katika eneo hilo bado juhudi mbalimbali zilikuwa zikiendelea kujaribu kuutoa mwili wa marehemu Johnson kutoka katika shimo hilo.

0 Responses to “ KIJANA MMOJA AFARIKI BAADA YA KUANGUKUWA NA JIWE”

Post a Comment

More to Read