Saturday, October 10, 2015
MWAMBUSI ASOGEA KABISA MLANGONI YANGA, KATIBU MKUU ASEMA WATATANGAZA JUMAPILI
Do you like this story?
Kila
kitu kinaenda vizuri kwa Kocha Juma Mwambusi kutua Yanga kumsaidia Hans van Der
Pluijm kuifundisha timu hiyo akichukua nafasi ya Charles Mkwasa aliyepata kazi
Taifa Stars.
Yanga
hadi sasa ina orodha ya makocha kadhaa waliotajwa kumudu kazi iliyokuwa
ikifanywa na Mkwasa, lakini taarifa zinasema Mwambusi anayeinoa Mbeya City
ndiye mwenye nafasi kubwa ya kupewa dili hilo.
“Pluijm
ndiye anayesubiriwa kutoa jibu lake juu ya msaidizi wake na Mwambusi anapewa
nafasi kubwa kutokana na uwezo wake hasa jinsi anavyoifunga Simba kila mara,”
kilisema chanzo chetu.
Alipotafutwa
Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ili atoe ufafanuzi kuhusu jambo hilo,
alisema: “Tuna majina ya makocha wengi na Jumapili (kesho) tutamtangaza
aliyekidhi vigezo na Jumatatu ataanza kazi.”
Mwambusi
mwenyewe amekuwa mgumu wa kutoa ufafanuzi kuhusu kuhusishwa kwake na Yanga
kwani mara kadhaa hapokei simu yake ikidaiwa yupo katika mazungumzo ya kina na
viongozi wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWAMBUSI ASOGEA KABISA MLANGONI YANGA, KATIBU MKUU ASEMA WATATANGAZA JUMAPILI”
Post a Comment