Tuesday, October 13, 2015

MAGUFULI 'AWAIBUKIA' NAPE, MEMBE


Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli (kushoto) akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye katika Viwanja vya soko la Majengo


Mama Salma Kikwete akiwaasa wakazi wa Lindi Mjini kumchagua Magufuli kwa maendeleo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Ntama (CCM) Mh. Bernard Membe akimpigia debe Magufuli Lindi Mjini katika viwanja vya Mpilipili.

Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa

Magufuli na Mama Salma Kikwete wakifurahia jambo.


Mgombea urais wa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Pombe Magufuli leo 'ameibukia' katika Mkoa wa Lindi kwa kufanya mikutano ya kampeni maeneo mbalimbali mkoani humo ikiwemo jimbo la Mtama lililokuwa likishikiliwa na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kabla ya kumuachia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye anayegombea ubunge wa jimbo hilo hivi sasa.

Baadhi ya maeneo na majimbo ambayo Magufuli alifanya kampeni hii leo ni Nachingwe katika Uwanjwa wa Sokoine huku mikutano mingine mikubwa zaidi ya Saba akifanya katika maeneo ya Chihola, Jimbo la Ruangwa, Jimbo la Mtama ambapo mkutano ulifanyika katika viwanja vya Soko la Majengo.

Baada ya hapo Magufuli alimalizia kampeni zake kwa leo katika mkutano ulihudhuliwa na umati mkubwa wa watu.

0 Responses to “MAGUFULI 'AWAIBUKIA' NAPE, MEMBE”

Post a Comment

More to Read