Tuesday, October 13, 2015

WANAHABARI WATAKIWA KUFUATA MAADILI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.




Katika kipindi  hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu wanahabari wametakiwa kuandika habari zao kwa kufuata maadili ya uandishi wa habari ili kuliepusha taifa na kuingia kwenye machafuko na uvunjifu wa amani.

Kauli hiyo imetolewa  na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya umoja wa vyama vya waandishi wa habari tanzania(UTPC) Bw.Andrew Kuchonjoma  wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau  wa habari na wanahabari mjini Songea mkutano uliobeba agenda ya  wanahabari na uchaguzi.

Kwa upande wake mmoja wadau wa habari mkoani Ruvuma ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwenye mkutano huo Bw. Frolence Kundi amesema habari ni kitu muhimu katika jamii na kwamba wanahabari mkoani ruvuma wamekuwa na mchango mkubwa katika kuripoti masuala ya uchaguzi.

0 Responses to “WANAHABARI WATAKIWA KUFUATA MAADILI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.”

Post a Comment

More to Read